Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yatoa samansi ‘afande’ afike mahakamani

Muktasari:

  • Mtuhumiwa huyo kwa jina maarufu la ‘Afande’ amefunguliwa shauri la malalamiko namba 23627 na Paulo Kisabo akidaiwa kutenda kosa la kubaka kwa kundi.

Dodoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imetoa wito wa kufika mahakamani (samansi) kwa Fatma Kigondo anayelalamikiwa kwa kosa la kubaka kwa kundi.

Mahakama imetoa samansi hiyo baada ya ile ya awali iliyomtaka kuhudhuria mahakamani leo Agosti 23, 2024 kutotekelezwa.

Shauri hilo la malalamiko namba 23627 limefunguliwa na Paulo Kisabo na lipo mbele ya Hakimu Mkazi Francis Kishenyi. Lilipangwa kwa kutajwa leo.

Wakili wa mlalamikaji, Peter Madeleka ameiomba mahakama kutoa utaratibu mwingine kwa kutoa amri ya kumkamata Fatma kwa kuwa alipata wito wa kuitwa mahakamani jana Agosti 22 lakini hakutokea.

Katika malalamiko hayo, Kisabo anamlalamikia Fatma akidai ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), akidai alishiriki kuratibu na kufanikisha ubakaji wa kundi.

“Kwa kuwa ni kosa la jinai na waliokuwa wakitakiwa kutimiza wajibu wao hawakufanya hivyo, ndiyo maana na sisi tuko hapa. Tunaomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa,” alidai Madeleka.

Ameiomba mahakama kutumia kifungu cha 130 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kumkamata Fatma anayedaiwa kuwa ni afande kwa kuwa malalamiko yao yanaangukia katika makosa ya jinai.

Hakimu Mkazi Kishenyi amesema kifungu hicho hakilazimishi mahakama kutoa amri ya kukamatwa pekee, bali pia kinatoa fursa ya kutoa hati ya wito.

“Nitatoa hati ya wito nyingine ili nijiridhishe kama hati ya wito tuliyoitoa jana haijamfikia,” amesema.

Ameahirisha shauri hilo hadi Septemba 5, 2024.