Mahakama yaamuru kesi ya Lissu isirushwe 'Live'
Mwenyekiti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu akizungumza na mawakili wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Mtandao
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeamuru kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, isirushwe moja kwa moja kama ilivyokuwa awali.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 18, 2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Francisco Kiswaga, kwa kile alichoeleza kuwa haki ya mashahidi wanaopaswa kulindwa bila kufanya hivyo watajukikana.
Endelea kufuatilia Mwananchi