Maduka 14 yateketea kwa moto

Muktasari:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu hiyo ilianzia kwenye baadhi ya majokofu.
Arusha. Hitilafu ya umeme imeteketeza kwa moto maduka 14 katika eneo la Mianzini jijini Arusha jana asubuhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu hiyo ilianzia kwenye baadhi ya majokofu.
Kamanda Mkumbo amesema baada ya hitilafu hiyo, moto huo ulishika mitungi ya gesi iliyolipuka na kuanza kusambaa kwa kasi na kuunguza maduka hayo.
Amesema wamefanikiwa kuokoa baadhi ya mali katika maduka tisa kati ya 14 kwa msaada wa wananchi na wasamaria wema waliokuwa katika eneo la tukio lakini ukubwa wa hasara bado haujajulikana.