Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madereva wanne ndani kwa kesi ya shambulio

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Madereva wanne wafikishwa katika Mahakama ya Mwanzo wakikabiliwa na shtaka la kudhuru mwili.

Dar es Salaam. Madereva wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo wakikabiliwa na shtaka la kumshambulia na kumdhuru kwa kumpiga Bakari Rashid.

Washtakiwa hao ni Omary Kabalimo mkazi wa Mbagara Kuu, Bahati Eliya mkazi wa Kimara, Elisha Kibanga mkazi wa Chamazi na Melkidea Silvanus mkazi wa Mbande.

Karani, Emmy Mwansansu akiwasomea hati ya mashtaka washtakiwa hao leo Mei 10, 2023 alidai washtakiwa hao walitenda kosa la shambulio na kumdhuru mwili.

Imedaiwa kuwa Mei 9, 2023 mtaa wa Samora wilayani Ilala, washtakiwa hao wakiwa maeneo hayo kinyume cha sheria walimpiga Rashidi sehemu za mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia maumivu.

Baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa wote kwa pamoja walikana kosa linalowakabili.

Ndipo Rashidi alieleza mahakama hiyo kuwa atakuwa na mashahidi watatu ambao watatoa ushahidi wao mahakamani hapo

Hakimu Mkazi Mfawidhi Claudis Kipande amesema washitakiwa watakuwa nje kwa dhamana endapo watatimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja kila mmoja atakayesaini bondi ya Sh200, 000.

Washitakiwa wote wameshindwa kutimiza masharti hayo hivyo wamepelekwa mahabusu na kesi hiyo imeahirishwa hadi Me 18, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji.