Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari bingwa fani za kipaumbele kupatikana ngazi za rufaa 2025

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Muktasari:


 Lengo la Serikali ifikapo Juni 2025 hospitali zote za rufaa ziwe na madaktari bingwa kwenye fani nane za kipaumbele
 

Geita. Serikali imesema imeweka lengo la kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 hospitali zote za ngazi ya rufaa ziwe na madaktari bingwa muhimu katika fani zote za kipaumbele.

Mabingwa waliotajwa kuhitajika ni madaktari bingwa wa wanawake, watoto, upasuaji wa mifupa ,dawa za usingizi na ganzi , upasuaji wa jumla, huduma za dharura, magonjwa  ya ndani pamoja na yule  wa mionzi.

Ili kufanikisha hilo, Wizara ya Afya imesema imeanza kusomesha madaktari 300, katika fani nane za kipaumbele lengo likiwa ni kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma za kibingwa.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo jana Machi 16, 2024 , wakati wa  ziara ya siku mbili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi ilipotembelea Mkoa wa Geita na kukutana na changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada za afya.

 “Tunao madaktari 300 wanasomeshwa na Serikali katika fani nane za kipaumbele na kwa sasa kwenye zile hospitali zenye madaktari zaidi tunawaondoa na kuwapeleka kwenye hospitali za rufaa zenye upungufu,” amesema Waziri Ummy.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo amesema kada ya afya ina upungufu wa watumishi kwa zaidi ya asilimia 50 na kuitaka Serikali  kuona namna watakavyofanya ikiwa ni pamoja na kuhamisha kwenye hospitali zenye idadi kubwa, kusomesha na kuajiri wahitimu walioko mtaani ili kupunguza changamoto hiyo.

Awali, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigella, Mkuu wa Wilaya ya Chato Said Nkumba amesema  mahitaji ya watumishi katika kada ya afya kwenye mkoa huo ni 5,874 na waliopo sasa ni 2,850 sawa na asilimia 48.5 ya uhitaji hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 3,024.

Nkumba amesema mkoa huo wenye wakazi milioni 2.9 mahitaji ya vituo vya kutolea huduma ni 582 na vilivyopo sasa ni 247 hivyo kuwa na upungufu wa vituo 372.

Ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vituo, tayari mkoa umeanza ujenzi wa vituo zaidi ya 300 vya zahanati na vituo vya afya ambavyo vikikamilika vitaongeza upatikanaji wa huduma kutoka asilimia 36 iliyopo sasa hadi kufikia 92.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa huo, Mfaume Kibwana amesema kutokana na huduma za kibingwa kuwepo kwenye hospitali hiyo, wamefanikiwa kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kutoka 24 mwaka 2022 hadi kufikia 16 mwaka 2023 na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 418 hadi 204 katika kipindi kama hicho.