Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Machimbo Musoma yaua wawili, wengine waokolewa, mmoja asakwa

Picha na Mtandao.

Muktasari:

  • Wachimbaji wadogo wa dhahabu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kunusurika huku mmjoa akiwa hajulikani alipo baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa dhahabu Kataryo wilayani Musoma, Mkoa wa Mara.

Musoma. Watu wawili wamefariki dunia huku wengine wawili wakiokolewa baada ya kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba dhahabu katika machimbo ya wachimbaji wadogo yaliyopo katika Kijiji cha Kataryo, wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, Aprili 4, 2026, Mkuu wa Wilaya ya Musoma (DC), Juma Chikoka amesema mbali na watu hao wawili kufariki na wengine wawili kuokolewa pia mtu mmoja bado hajulikani alipo hivyo juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Amesema tukio hilo limetokea  wakati wachimbaji hao watano walipoingia katika duara (shimo) moja kwaajili ya kufanya shughuli zao kisha kifusi kuporomoka na kuwafukia wakiwa ndani  wakiendelea na shughuli zao.

"Taarifa za awali zinasema walikuwa watu watano na baada ya tukio wawili wametolewa wakiwa hai na wawili wakiwa wamefariki ambapo mmoja bado hajapatikana,juhudi za kumtafuta zinaendelea," amesema.

Chikoka amesema shimo hilo lililohusika katika ajali hiyo ni miongoni mwa mashimo ambayo yaliwekewa alama kwaajili ya kuzuia shughuli za uchimbaji kutokana na masuala ya kiusalama lakini  wachimbaji hao waliamua kufanya shughuli zao kinyume cha utaratibu.

"Shimo hilo liliwekewa alama kuzuia shughuli za uchimbaji baada ya kubainika kuwa sio salama na wachimbaji wote walikuwa wanalijua hili,  lakini wenzetu hawa hawakulizingatia hilo walipoona viongozi wameondoka wao wakaamua kuingia na kuendelea na shughuli zao," ameongeza 

Amesema taarifa ya kina ataitoa baada ya kupata taarifa kutoka ofisi ya madini mkoa wa Mara sambamba na kumalizika kwa shughuli ya utafutaji wa mtu huyo ambaye bado hajapatikana.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara,  Agostino Magere amesema tukio hilo limetokea leo Jumamosi, Aprili 4, 2026 wakati wachimbaji hao wakiendelea na shughuli zao.