Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabasi ya shule kuwa na mhudumu wa kike, kiume

School bus

A safer school transport system is the responsibility of diverse stakeholders, not just schools and parents.

Photo credit: File

Muktasari:

  • Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetaka mabasi yanayosafirisha wanafunzi kuwa wa mhudumu wa kike na kiume.

Dar es Salaam. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imewataka wamiliki wa shule wanaotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi kuwa na mhudumu wa kike na wa kiume kwenye kila gari.

Agizo hilo limetolewa limetolewa na wizara hiyo kupitia waraka wake uliosainiwa na Kamishna wa Elimu, Dk Lyabwene Mutahaba.

Kulingana na waraka huo, mmiliki wa shule atakayeshindwa kutekeleza hilo, anapaswa kutoa taarifa ya sababu ya kushindwa kwa wathibiti ubora.

"Endapo itashindikana kabisa mhudumu wakike atumike kutoa huduma kwenye gari husika baada ya kutoa taarifa kwa mthibiti ubora wa shule," umeeleza waraka huo.

Utekelezaji wa maelekezo hayo, kwa mujibu wa waraka huo unapaswa kuanza kabla ya muhula wa pili wa masomo kwa mwaka 2023.

Maelekezo mengine ni kuacha kuweka miziki, picha na video zinazokwenda kinyume na maadili na badala yake, ziwekwe zinazojenga maadili na uzalendo kwa wanafunzi.

"Kumkomesha vitendo vya ukatili kwa wanafunzi wanapokuwa kwenye mabasi na kuwa na ratiba rafiki za safari ili wanafunzi hususan watoto wadogo wapate muda wa kutosha wa kupumzika," umeeleza waraka huo.

Waraka huo, umeelekeza magari yote yanayosafirisha wanafunzi yanapaswa kuwa na vioo angavu na watumishi kwenye usafiri wawe waaminifu.