Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabaraza ya ardhi ya kata, vijiji yapigwa marufuku kutoa hukumu

Muktasari:

Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula  amepiga marufuku kwa mabaraza ya aridhi ya kata vijiji kutoa hukumu ya kesi za aridhi kwenye maeneo yao badara yake yanatakiwa kutoa usuluhishi.

Sengerema. Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula  amepiga marufuku kwa mabaraza ya aridhi ya kata vijiji kutoa hukumu ya kesi za aridhi kwenye maeneo yao badara yake yanatakiwa kutoa usuluhishi.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu Machi 21, 2022 wilayani Sengerema alipokuwa akizindua Baraza la Aridhi la Wilaya ya Sengerema.

Amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi juu ya mabaraza ya aridhi na kata na vijiji kutoa hukumu zisizo za haki na kuleta mkanganyiko.

"Kesi zote za aridhi zitahukumiwa na Baraza la Aridhi la Wilaya na siyo mabaraza ya aridhi ya kata au vijiji, baraza la aridhi la wilaya ndiyo lina mamlaka hayo kisheria " amesema Mabula.

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu kwenye mikutano yake ya hadhara kwa nyakati tofauti alisisitiza kuwa atahakisha Wilaya ya Sengerema inapata baraza la aridhi la wilaya ili kuwasaidia wananchi wa Sengerema na Buchosa kupata huduma ya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amesema watasimamia mabaraza hayo ili yaweze kutenda haki kwa kufuata taratibu na sheria za nchi.