Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lifahamu tairi la gari unalotumia

Lifahamu tairi la gari unalotumia

Muktasari:

  • Ili kujiweka salama katika safari kila dereva anapaswa kulifahamu vema tairi analotumia, hasa muda wake wa matumizi, uzito unaostahili na kasi linaloweza kuhimili.

  


Dar es Salaam. Ili kujiweka salama katika safari kila dereva anapaswa kulifahamu vema tairi analotumia, hasa muda wake wa matumizi, uzito unaostahili na kasi linaloweza kuhimili.

Kwenye kila tairi kumeandikwa mambo yote yanayotoa mwongozo kama muda wa matumizi, mazingira ambayo tairi linapaswa kutumika, kiwango cha mwisho cha mwendo kasi, uzito na kiwango cha upepo kinachopaswa kuwekwa.

Mambo mengine ambayo yameainishwa katika tairi ni muundo wake ilivyotengenezwa na namna ya kupima iwapo tairi limeisha.

Mkuu wa Usalama Barabarani katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis Dar es Salaam, ASP Ibrahim Samwix anasema katika kila tairi kumeandikwa maandishi DOT, NAA au DFK na kisha namba mfano 2408, hivyo linaweza kusomeka ‘DOT 2408’ maana yake imetengenezwa wiki ya 24 mwaka 2008, hivyo kuanzia hapo inatakiwa kutumika kwa miaka minne hadi sita tangu itengenezwe.

“Kwa mujibu wa watengenezaji, matairi mengi yana uwezo wa kukaa kwa muda wa miaka mitano mpaka sita tangu siku limetengenezwa, lakini hata lisipotumika, bado muda wake wa matumizi utasalia uleule.

“Hivyo baada ya miaka sita, tairi hilo halitatakiwa tena katika matumizi,” anasema.

Anasema kuna namna mbili za kujua kuwa tairi limeisha hata kama lipo ndani ya muda wa matumizi – kuna aina ya tairi ambazo unaweza kujua kuwa zimeisha kwa kashata zake kufikia usawa wa vinundu vilivyopo katikati na baadhi ya matairi yana kishimo ambacho ukitumbukiza vernier caliper (kipimo), unene wake unatakiwa usiwe chini ya milimita 2.

Mbali na kwisha kwa tairi na kupita kwa muda wa matumizi, tairi linaweza kukosa sifa za kufaa kwa matumizi kama limechanwa na kitu na athari zake zikafika sehemu ya ndani, kwa kuwa hilo linaweza kupasuka muda wowote.

Ufanye nini kabla ya safari

Mkurugenzi wa Evolution Garage iliyopo Kamata jijini Dar es Salaam, Alex Evodius anashauri mambo matatu muhimu kwamba tairi lazima liwe sahihi kwa ukubwa unaotakiwa, liwe limejazwa upepo sawia, lisiwe na aina yoyote ya uharibifu.

“Kutumia tairi zenye hitilafu yoyote ni kukiweka chombo chako rehani, kwa kuwa tairi ni moja ya nyenzo muhimu kwa chombo chako, hitilafu moja inaweza ikasababisha ajali,” alisema Evodius.

Vilevile alisema kuna aina za matairi zinatakiwa kulingana na mazingira, hivyo ni muhimu sana kwa watumiaji na wamiliki wa magari kufahamu aina za matairi wanayoyahitaji kulingana na mazingira watakapoyatumia.

Anasema kuna, matairi ya kipindi cha baridi ambayo yana sifa za kutumika katika mazingira ya barafu na yale ya kiangazi zinayotumika zaidi katika mazingira ya joto.