Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kodi ya jengo yapaa, kuanza kutozwa mwezi Julai

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo imetangaza kuanza kwa viwango vipya vya ulipaji wa kodi ya majengo, ambao utawalazimu wamiliki nchini kulipa kiwango cha juu zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo imetangaza kuanza kwa viwango vipya vya ulipaji wa kodi ya majengo, ambao utawalazimu wamiliki nchini kulipa kiwango cha juu zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Mabadiliko mapya ni ya ukusanyaji wa kodi ya majengo, ambayo hulipwa kupitia ununuzi wa tokeni za umeme.

Hii inafuatia marekebisho ya Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (Ukadiriaji) (SURA 289) yaliyofanywa kupitia Sheria ya Fedha ya 2023.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo Julai 25, 2023; TRA imeeleza kuwa viwango hivyo kwa mwaka vitakuwa ni Sh18,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja, kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kile cha Sh12,000 kilichokuwa kikitozwa hapo awali.

Kwa upande mwingine, mmiliki wa jengo la ghorofa moja katika miji, halmashauri za manispaa na majiji, yeye atatozwa Sh90, 0000 kutoka Sh 60, 000 kwa mwaka.

Hata hivyo, kwa upande wa halmashauri za wilaya, nyumba za ghorofa, bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa Sh90, 000.

Kwa mujibu wa TRA kila mnunuzi wa umeme atakatwa Sh1, 500 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Sh7, 500 kwa mwezi kwa jengo la ghorofa.

Serikali ilianza utekelezaji wa malipo haya ya kodi ya majengo kupitia manunuzi ya tokeni za umeme toka Julai 2021.