Kiwanda cha nguo Morogoro chateketea

Muktasari:
Meneja wa kiwanda hicho, Clement Munisi amesema moto huo umetokea leo saa 12 asubuhi baada ya mashine hiyo kulipuka na kuwashinda wafanyakazi na uongozi.
Morogoro. Kiwanda cha nguo cha 21st Century cha mkoani Morogoro kimeteketea kwa moto uliowaka kwa zaidi ya saa sita huku chanzo kikidaiwa ni mashine moja ya kufuma nyuzi kupata hitilafu na kulipuka.
Meneja wa kiwanda hicho, Clement Munisi amesema moto huo umetokea leo saa 12 asubuhi baada ya mashine hiyo kulipuka na kuwashinda wafanyakazi na uongozi.
Hata hivyo, Munisi amesema hasara iliyopatikana kutokana na moto huo bado haijafahamika lakini baadhi ya marobota ya vitambaa vilivyokuwa vikiandaliwa kwa ajili ya kutengeneza kanga, vitenge na mashuka yameokolewa.
Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro, Ramadhani Pilipili amesema moto huo umechukua muda mrefu kuzimwa kutokana na miundombinu ya kiwanda hicho ambayo haikuzingatia majanga ya moto.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz