Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kimeumana bungeni, Mulugo ataka baraza la mawaziri livunjwe

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa zamani, Philip Mulugo

Muktasari:

  • Mjadala wa taarifa za Kamati za Bunge juu ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali (CAG), umewaka moto bungeni baada ya wabunge kuonyesha hasira zao kwa kile kilichoelezwa Serikali kutowashughulikia mafisadi.

Dodoma. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa zamani, Philip Mulugo amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuvunja Baraza la Mawaziri kesho.

Mulugo ameyasema hayo leo Ijumaa Novemba 3, 2023 wakati wakichangia taarifa za kamati za Bunge za kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2022.

Taarifa hizo ni za kamati za kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Amehoji kwanini Serikali haitaki kuwawajibisha watu walioiba fedha na kwamba wananchi hawana mahali pa kuhoji wanategemea wabunge wawasemee.

Mbunge huyo wa Songwe (CCM), amesema kama wabunge wanataka kuweka historia ya Bunge na kwamba yeye haoni wivu kwa sababu ameshawahi kuwa Naibu Waziri na hata wakimrejesha kesho anaweza kufanya kazi nzuri.

“Mheshimiwa Mwenyekiti mimi ninajiamini hakuna kikingine ni kuchukua hatua tu leo mambo yanaenda ovyo ovyo namna hii haiwezekani mheshimiwa,” amesema na kuongeza;

“Sio kwamba ninaona wivu sababu mimi nilikuwa huko, nataka kurudi Hapana, lakini tulipofikia ni pabaya hii nchi inakufa sasa na nyie mnaotakia kuwajibisha watu hamtaki kuwawajibisha wanafanya kazi mawaziri wawili tu,” amesema.

Amesema anaonekana Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohammed Mchengerwa na kuhoji wengine wanafanya nini.

“Yaani fedha zinaliwa hivi hivi tunaenda kukamata wenye kesi za ngombe na kuku mitaani, mawaziri mnakuja hapa mnajibu atakayefanya hivyo watachukuliwa hatua nyie mbona mnashindwa kuchukua hatua?” amehoji.

Hatua hiyo ilimfanya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene kuomba kutoa taarifa, jambo ambalo alikubaliwa.

Akitoa taarifa hiyo, Simbachawene amesema Serikali ya awamu ya sita ndio imefanya kazi kuliko Serikali nyingine zote zilizopita na kwamba kama kuna Mbunge ambaye atashindwa kurudi bungeni atashindwa kwa sababu zake.

“Kesi ambazo ambazo zimefunguliwa na Serikali hii kutokana na watu wabadhirifu kutoka mwaka 2021 hadi Juni 2023 ni kesi 1,790 na katika kesi hizo, 963 Serikali imeshinda na watu wameshtakiwa,” amesema.

Akitoa taarifa kwa Mulugo, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka amesema kuwa walio wadogo zao mawaziri ndio waliofanya makosa na kuhoji kwa nini hawataki kujipambanua na kusema idadi ya wahalifu aliyonayo na muda anaotegemea kuchukua hatua ili mambo hayo yakome.

“Kwa nini...hapa tamkeni kanuni ya kushughulika na mafisadi tutakuwa pamoja…na nyinyi sio sehemu lakini mkinyamaza watu watashindwa kuwatofautisha wataona na nyinyi ni wabia,” amesema.