Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete: Samia akichaguliwa tena Taifa litaendelea kupata maendeleo makubwa

Muktasari:

  • Anasema anatamani katika uchaguzi mkuu huo utakaofanyika Oktoba, mwaka huu, wabunge na madiwani wengi watokane na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Bagamoyo. Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amesema Rais Samia Suluhu Hassan akichaguliwa tena katika uchaguzi mkuu ujao, Taifa litapiga hatua kubwa zaidi katika maendeleo.

Na amesema anatamani katika uchaguzi mkuu huo utakaofanyika Oktoba, mwaka huu, wabunge na madiwani wengi watokane na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kiwete ameyasema hay oleo Alhamisi Aprili 10, 2025 katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika shule ya amali inayojengwa katika kijiji cha Msoga, mkoani Pwani na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ismail Ussi.

“Sijui kama watasema natumia Mwenge kuzungumzia hili, lakini binafsi natamani Rais Samia achaguliwe tena na vilevile ningependa wabunge na madiwani watoke CCM,” amesema Kikwete.

Muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo hilo ulipokuwa unapokelewa Mwenge wa Uhuru, Rais Kikwete alitembelea pia majengo yanayoendelea kujengwa na amepanda mti wa kumbukumbu kwenye eneo hilo la shule.

Pia alikabidhi hati ya ardhi ya eneo linalojengwa shule hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge ambaye aliikabidhi rasmi kwa uongozi wa Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumzia historia ya eneo hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 400, Rais mstaafu Kikwete amesema awali, lilitolewa kwa watu kutoka Marekani waliokuwa na nia ya kujenga chuo, lakini walishindwa kutekeleza mradi huo na kuondoka.

“Kuna watu kutoka Marekani waliliomba hili eneo, waliruhusiwa, lakini baadaye walitokomea. Serikali ilipoamua kulitumia upya, tulikubaliana litumike kwa manufaa ya wananchi,” amesema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ussi amesisitiza umuhimu wa kulitumia vyema eneo hilo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Nimepokea hati kutoka kwa Rais mstaafu na nimekabidhi kwa uongozi wa halmashauri. Nawaomba mtumie eneo hili kwa malengo yaliyokusudiwa, tayari shule inajengwa hapa naimani na huduma zingine za kijamii majengo yake yatajengwa hapa,” amesema Ussi.

Mkazi wa Chalinze, Abeda Jumaa amesema ujenzi wa shule hiyo katika eneo hilo ni ukombozi mkubwa kwao.

Amesema matumaini ya vijana kupata elimu ya amali (ufundi), itawapatia fursa vijana wengi wa ndani nan je ya eneo lao kujifunza maarifa ya kujitegemea.

Ukiwa katika Halmashauri ya Chalinze, Mwenge wa Uhuru umetembelea, kukagua na kuzindua jumla ya miradi saba yenye thamani ya Sh28.9 bilioni.