Kibaha watakiwa kuandaa mashamba kabla ya mvua

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Balang'alalu iliyopo wilaya ya Hanang', mkoa wa manyara, wakipalilia mahindi kwenye shamba la shule jana.mahindi hayo yakivunwa hutumiwa kwa chakula shuleni hapo
Muktasari:
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba ambaye alisema kutonyesha mvua za vuli katika msimu uliopita kusiwakatishe tamaa na kusababisha kutojihusha na masuala ya kilimo.
WAKAZI wa wilayani Kibaha mkoani Pwani, wamekumbushwa kuandaa mashamba mapema ili kwenda sanjari na msimu wa mvua zinazotarajia kuanza kunyesha wakati wowote kuanzia sasa.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba ambaye alisema kutonyesha mvua za vuli katika msimu uliopita kusiwakatishe tamaa na kusababisha kutojihusha na masuala ya kilimo.
Kihemba alisema kuwa kilimo ni moja ya njia inayoweza kumkomboa mkulima hasa katika suala la bajeti ya chakula, hivyo ni vyema wakazi hao wakazingatia na kufuata taratibu na kanuni zinazotakiwa juu ya kilimo.
“Msimu wa mvua za vuli haukuwa mzuri kwa mwaka uliopita, lakini hicho kisiwe kikwazo na sababu ya kufanya kusiwe na maandalizi ya kilimo katika msimu huu unaotarajia kuanza wakati wowote naomba tujitahidi kuandaa mashamba yetu ili mvua zitakapoanza kunyesha yawe safi tayari kwa kilimo,”alisema.
Aliwataka wakazi hao kujikita zaidi katika kilimo cha mazao ambayo yameonekana kustawi katika ardhi ya kibaha ambayo ni pamoja na mihogo, ufuta, alizeti mtama pamoja na mbogamboga.
Alisema wakulima wengi wilayani humo wanalima kwa mazoea kulingana na mazao wanayoyataka bila kujali faida na hasara zinazotokana na hali hiyo hivyo aliwataka kubadilika ili waendane na hali inayotakiwa.
Kibaha ni moja ya Wilaya za Mkoa wa Pwani iliyojaliwa kuwa na maeneo makubwa ya ardhi lakini
sasa mapori kutokana na wakazi wengi kutojihusha na kilimo.