Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KESI YA MJANE WA BILIONEA MSUYA: Shahidi aliyefundishwa na FBI alipokutana na wakili Kibatala kizimbani

Wakili Peter Kibatala (kushoto) akiteta jambo na mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Steven Mrita (wa pili kushoto) katika chumba cha Mahakama Kuu. Picha na Sunday George.

Muktasari:

  • Shahidi wa 17 katika kesi inayomkabili mjane wa Bilionea Msuya, na mwenzake ameeleza jinsi alivyofanya ukaguzi eneo la tukio la mauaji ya mdogo wa Bilionesa Msuya.

Dar es Salaam. Kesi ya mauaji ya Aneth Msuya, mdogo wa marehemu Erasto Msuya, aliyekuwa mfanyabiashara maarufu madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya, leo Agosti 18, 2023 imeelendelea kuunguruma Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Hii ni kesi namba 103 ya mwaka 2018 inayomkabili mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Steven Mrita na mwenzake Revocatus Everist Muyella, maaruf kama Ray, wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo ya Aneth.

Aneth aliuawa Mei 25, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam miaka mitatu tangu kuuawa kwa kaka yake, Bilionea Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Agosti 7, 2013.

Leo Mahakama hiyo imepokea ushahidi wa shahidi wa 17, Ditektivu Sajent John Bernard Mwambusi, kutoka Kitengo cha Uchunguzi wa Sayansi Jinai (Forensic Science Investigation) Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Temeke, chini ya Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.

Ndiye shahidi aliyefanya ukaguzi eneo eneo la tukio na kukusanya vielelezo katika eneo hilo la tukio kikiwemo kisu kilichodhaniwa kuwa ndicho kilichotumika katika mauaji.

Katika ushahidi wake ameelezea kwanza ameelezea utaalamu wake, majukumu yake, hali aliyoikuta eneo la tukio, alivyofanya ukaguzi vielelezo alivyovipata mnyororo wa utunzaji wa vielelezo hivyo hadi alipovikabidhi kwa mwenesha mashtaka.

Hata hivyo baada ya maelezo ya ushahidi wake huo alikumbana na maswali ya dodoso kutoka kwa wakili wa utetezi, Peter Kibatala ambaye amembana kuhusiana na taratibu za utendaji wake, ukusanyaji na uhifadhi wa vielelezo hivyo kama alizingatia matakwa ya kisheria.

Ufuatao ndio ushahidi wake wa msingi wakati akiongozwa na mwendesha mashtaka, pamoja na mahojiano baina yake na wakili Kibatala.


Ushahidi mkuu

Akiongozwa na mwendesha mashtaka,Wakili wa Serikali Mwandamizi  Paul Kimweri, shahidi huyo kwanza aliieleza mahakama kuwa Mimi anafanya kazi Polisi kama mtaalamu wa Ukaguzi wa matukio katika kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi Jinai (Forensic Science Investigation)

Hiyo ni idara inayojihusisha na uchunguzi wa kisayansi ya jinai, kuhusu silaha, nyaraka na vinasaba vya binadamu (DNA).

Kwa mujibu wa maelezo yake amefanya kazi katika idara hiyo kwa miaka 32 na amepata utaalamu huo kutoka Taasisi ya Upelelezi ya Shirikisho la Marekani ya FBI (Federal Bereau of Investigation) na kutoka kwa Waturuki.

Katika mafunzo ya FBI yaliyoendeshwa katika Chuo cha Polisi Kurasini, mwaka 2002 yalihusu ukaguzi wa matukio na kupiga picha, na alipata cheti yaani Certificate in Crime Scene Investigation.

Mwaka 2012 alipata mafunzo kutoka Uturuki kuhusu ukusanyaji wa vielelezo kutoka eneo la ambayo pia yalifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es Salaam, na baada ya mafunzo alipata chetu yaani Certificate in Collection Evidence Method.

Katika eneo la tukio huwa anakusanya vielelezo ambavyo vinaweza kusaidia kuunganisha kosa lililotendeka na mtuhumiwa na mara nyingi vinategemea na kosa mathalan tukio la silaha, nyaraka au mauaji.

Vifaa vinavyotumika wakati wa kufanya ukaguzi eneo la tukio ni pamoja na mipira ya kuvaa mikononi (gloves) barakoa, vitakasa mikono (sanitizer) koti maalum; kontena na bahasha kama vifungashio vya vielelezo na whitepowder.

Alitangazwa katika Gazeti la Serikali la (GN) namba 416 la mwaka  mwaka 2014  kuwa Afisa mpelelezi mtaalamu wa kukusanya vielelezo eneo la tukio.


Siku ya tukio

Mei 26 , 2016 muda wa saa moja  asubuhi akiwa  ofisini Chang'ombe, kituo cha Polisi, mkuu wake wa kazi, Mkuu wa  Upelelezi Mkoa wa Temeke (RCO) Richard Mchomvu  alimtaka  aende kukagua eneo la mauaji Kibada, Kigamboni.

Hivyo alichukua kisanduku (Kitbox) lenye vifaa vya kazi aakaondoka akiwa ameambatana na RCO Mchomvu mpaka Kibada katika nyumba lilikokuwa limetokea tukio hio la mauaji, ambapo walikuta Polis tayari wameshaweka utepe katika geti la nyumba hiyo huku kukiwa na watu wengi waliokuwa wamefika kushuhudia tukio hilo.

Yeye pamoja na RCO Mchomvu waliingia kwenye geti wakamkuya Mkuu wa Upelelezi Wilaya (OC-CID) ya Kigamboni, akiwa askari mwingine nje mbele ya nyumba, ambao walimwelezea kuhusu kuwepo tukio hilo la mauaji.

Baada ya kupata maelezo mafupi alianza kukagua kuanzia mlango wa sebuleni, ambao ulikuwa umevunjwa. Aliendelea kukagua chumba baada ya chumba ambapo niligundua vipande vikubwa vya matofali.

Aliingia kwenye chumba ambacho alikuta mwili wa marehemu, ukiwa hauna nguo, ukiwa uchi na damu nyingi ikiwa imetapakaa sakafuni, huku ukiwa na jeraha la kitu cha ncha kali kwenye koo.

Pembeni ya mwili alikuta kisu chembamba chenye mpini mweusi kilichokuwa na damu, pembeni ya kitanda alikuta chupi yenye rangi ya zambarau iliyokuwa imejiviriga pamoja na filimbi ya chuma yenye rangi silver.Pia baadhi baadhi ya nguo hazikuwa katika mpangilio mzuri.

Baada ya hapo alibadilisha gloves alizokuwa amevaa akavaa nyingine, akachukua kielelezo cha kisu akakiweka kwenye bahasha ya khaki na kufunga kwa lakiri ya rangi nyekundu,

Bahasha ilikuwa na maandishi forensic service. Aliandika herufi A juu ya bahasha hiyo kama alama ya kielelezo hicho.

Kisha alivua gloves hizo akatakasa mikono kwa nikasanitizer, akavaa gloves nyingine akaendelea na kielelezo kingine ambapo aaliokota cha chupi akakifunga kwenye bahasha kwa lakiri, akaainisha kwa alama B kwamba chupi.

Alibadilisha tena gloves akaokota kielelezo ambacho ni filimbi akatia kwenye bahasha akakitambulisha kwa kuweka alama C.

Sababu za kuchukua vielelezo hivyo kwanza kisu kwa sababu alikuta mwili wa marehemu una jeraha shingoni kwa hiyo aliona kinaweza kumsaidia katika uchunguzi wake wavinasaba.

Alichukua chupi kwa kuwa alikuwa anataka kujua endapo marehemu aliingiliwa na alichukua filimbi kwani alitaka kujua kama marehemu aliitumia kupuliza ili kuomba msaada.

Baada ya kukusanya vielelezo hivyo alivipeleka katika kituo cha Polisi Kigamboni, ambako alimkuta WP (askari wa kike) Mwaka akiwa katika chumba cha kuhifadhia vielelezo, hivyo akamkabidhi vielelezo hivyo.

Agosti 28, 2016 RCO Mchomvu alimtuma kwenda kuchukua vielelezo Kigamboni ambapo aliokabidhiwa na WP Mwaka akavipeleka ofisi ya RCO Temeke akamkabidhi WP Elentruda, ambaye alimkuta tayari akiwa PF180 (Fomu ya Polisi ya kujaza vielelezo) akajaza huku yeye akimtajia kila kilichokuwemo katika bahasha husika.

Kesho yake Agosti 29, 2016, RCO Mchomvu alimtuma kupeleka vielelezo hivyo makao makuu ya Polisi na aliambatana na Elentruda, ambaye ndiye aliyevikabidhi kwa kuwa ndiye aliyekuwa amevibeba

Machi 15, 2017 alitumAa na RCO Mchomvu akaenda ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua ripoti pamoja na vielelezo hivyo.

Huko alikabidhiwa vielelezo hivyo na Segumba, yaani kisu, chupi pamoja na filimbi, vikiwa na bahasha ya khaki na lakiri na utepe wa ofisi ya Mkemia.

Dk Fidelis Segumba ni shahidi wa 15 katika kesi hiyo. Huyu Mkemia na wakati huo alikuwa meneja wa maabara ya uchunguzi wa kisayansi jinai Baiolojia na vinasaba.

Ndiye aliyefanya uchunguzi wa uhusiano wa kivinasaba katika vielelezo hivyo vilivyopatikana eneo la tukio na vinasaba katika mpanguso wa ndani ya shavu (chembechembe za mate) ya mshtakiwa wa pili, Muyella

Hivyo baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na vielelezo hivyo alirejea navyo ofisini na ripoti ya uchunguzi wa vielelezo hivyo akamkabidhi RCO Mchomvu.

Vile vielelezo alivitunza katika kaski la ofisi ya Forensic likiwa chini ya uangalizi wake mwenyewe mpaka Agosti 15, 2023, alipovipeleka mahakamani kwa mwendesha mashtaka.


Kilio kilivyosimamisha mwenendo kwa muda

Wakati shahidi huyo anaelezea mazingira ya eneo la tukio vitu alivyovikuta mle ndani na hasa hali ya mwili wa marehemu alivyoukuta sakafuni, maelezo yake yalimfanya mmoja wa dada wa marehemu aliyekuwepo mahakamani hapo kushindwa kuhimili hisia za uchungu hivyo akajikuta anaangua kilio mahakamani hapo.

Kwanza alianza kulia kimyakimya huku akifuta machozi kisha akainama na kadri shahidi huyo alivyokuwa anaendelea mara alianza kulia kwa sauti ya chinichini lakini baadaye akaangua kilio kwa sauti ya juu hali iliyosababisha Mahakama kusimama kwa muda.

Askari Magereza mmoaja alimchukua na kumtoa nje ya ukumbi wa mahakama ambako aliendelea kulia kwa sauti mpaka mmoja wa askari Magereza aliyekuwemo ukumbini kumsaidia kushuka chini kabisa kutoka ghorofa ya kwanza inakosikilizwa kesi hiyo.

Baada ya hali hiyo kutulia ndipo kesi ilipoendelea tena na shahidi huyo akamalizia ushahidi wake.


Shahidi ana kwa ana na Wakili Kibatala

Baada ya shahidi huyo kumaliza ushahidi wake huyo mkuyu alikabiliwa na kibarua cha kujibu maswali ya dodoso kutoka kwa wakili Kibatala ambaye alilenga kupima uimara wa ushahidi wake.

Katika maswali yake, Wakili Kibatala alieleza zaidi katika taratibu zinazosimamia ukusanyaji na mnyororo wa uhifadhi wa vielelezo hivyo tangu kutoka eneo la tukio mpaka vinapofikishwa mahakamani, kama shahidi huyo alizingatia matakwa ya kisheria.


Hii ni sehemu tu na maswali ya wakili Kibatala na jinsi shahidi huyo mtaalamu na mzoefu alivyoyajibu.

Kibatala: Shahidi ni sahihi kwamba matendo yako yote yanaongozwa na sheria?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Unaifahamu fomu namba 118 (Scene of Crime Articles for Examination Book)?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unaifahamu fomu Namba 137, kitabu cha risiti za vielelezo?

Shahidi: Siifahamu

Kibatala: Unaifahamu PF (Police Form) 16 exhibit register?

Shahidi: Sizikumbuki

Kibatala: Nini kitakukumbusha?

Shahidi: Mimi siyo mtunza vielelezo

Kibatala: Unaifahamu exhibit label PF145?

Shahidi: Naifahamu.

Kibatala: Inahusiana na nini?

Shahidi: Inaonesha tarehe ya kesi na IR.

Kibatala: Ni kweli inaonesha kizibiti kinapotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine?

Shahidi: Mimi sikumbuki

Kibatala: Kielelezo kinapoingia exhibit room (chumba cha vielelezo) au kutoka, PF 145 huwa inajaza au haijazwi?

Shahidi: Sidhani kama inajazwa

Kibatala: Kielelezo kinapoingia fomu gani huwa inajazwa?

Shahidi: Unamkabidhi mtunza vielelezo

Kibatala: Unapochukua kizibiti eneo la tukio ni kweli inatakiwa kufunga lebo fulani?

Shahidi: Mimi sifanyi hivyo.

Kibatala: PGO (Mwongozo wa Utendaji Kazi wa Jeshi la Polisi unaifahamu?

Shahidi: Baadhi ya vifungu navifahamu

Kibatala: Kwa hiyo at least unaifahamu kuwa ipo. Sasa nakusomea PGO 229(9).   ….afisa anayepeleleza tukio lazima aweke lebo kwenye kila kizibiti, hili sharti unalifahamu?

Shahidi: Mimi hilo halinihusu

Kibatala: Mimi nakuliza unalifahamu?

Shahidi: Silifahamu

Kibatala: Ulisema kuwa ulikusanya kielelezo aina ya chupi. PGO 229(11), inayotaka kufunga lebo kwenye kizibiti aina ya nguo ifungwe (lebo) kwa uzi, unafahamu hilo sharti?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Shahidi ulionesha vidhibiti kadhaa ulivyosema ulivikusanya eneo la tukio, ambavyo uliviweka kwenye bahasha, unafahamu kwamba exhibit label haitakiwi kuwa juu ya bahasha bali kwenye kielezo husika chenyewe?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Wakati unatoa ushahidi ulimwambia Jaji kwamba wakati unakambidhi WP Mwaka vielelezo mliandikishana popote?

Shahidi: Nakumbuka nilimwambia

Kibatala: Mwambie Jaji ni kitabu gani?

Shahidi: Hapo sikumbuki

Kibatala: Bila kujali kama ulikitaja au hukukitaja, ulimwambia Jaji kwamba mlisaini kwenye hicho kitabu?

Shahidi: Mimi sisaini anasiami Mwaka

Kibatala: Ulimwambia Jaji kuwa Mwaka alisaini?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulisema ulipiga picha mle chumbani hali ilivyokuwa, kwa nini ilikuwa muhimu kupiga hizo picha?

Shahidi: Kuonesha hali ya tukio ilivyokuwa

Kibatala: Hizo picha ulipiga kwa utashi wako au kwa maelekezo ya RCO?

Shahidi: Kwa elimu niliyofundishwa

Kibatala: Hizo picha umezileta hapa angalau kuona hali ilivyokuwa?

Shahidi: Sijazileta lakini zipo

Kibatala: Ulisema ulifundishwa na FBI, Wamarekani ambao wako makini sana katika uchunguzi, walikwambia kuwa ni muhimu kuchukua (alama za vidole) fingerprint?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Ulisema ulikuta kisu kikiwa na damu, inaweza kuwa kuna mtu mwingine akawa amekishika, ulichukua fingerprint kwenye hicho kisu?

Shahidi: Kisu kilikuwa na damu uanachukuaje fingerprint?

Kibatala: Ulisema kwenye kit yako kulikuwa na whitepowder, kazi yake ni nini?

Shahidi: Kuchukulia fingerprint

Kibatala: Mimi nakuuliza hivyo maana najua ninachokuliza

Kibatala: Ulisema kulikuwa na vipande vya tofali haliwezi kujibeba lazima libebwe na mtu, na kwamba kulikuwa na nguo na makaratasi yaliyokua yametapakaa ulichukua fingerprint?

Shahidi: Sikuchua

Kibatala: Ulikuta mlango umevunjwa, je ulichukua fingerprint kwenye huo mlango?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulisema ulikuta kisu kina damu na damu ikiwa imetapakaa, uliwahi kuchukua sehemu ya damu hiyo chini kupeleka kwa Pathologist kujua kama damu.iliyoko kwenye kisu ndio hiyo ya marehemu Aneth kama.kisu hakijapandikizwa tu na mtu mwingine?

Shahidi: Mimi nilipeleka kisu kwa Mkemia

Kibatala: Mkemia hawezi kujua hilo

Kibatala: Shahidi uliwahi kusema hapa mahakamani kwamba ile chupi ilikuwa na damu?

Shahidi: Sijasema

Kibatala: Kwa hiyo kwa ujumla wake hakuna alama zozote za vidole ambazo zilichukuliwa eneo la tukio?

Shahidi: Hakuna