Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KESI YA MJANE WA BILIONEA MSUYA: Mshtakiwa atoa taarifa ya utetezi atakaoutoa

Miriam Mrina, mjane wa Bilionea Msuya 

Dar es Salaam. Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji Aneth Msuya; ameiarifu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, aina ya utetezi atakaoutoa ambao ni ule wa kutokuwepo eneo la tukio, kwa tarehe husika ya tukio hilo.

Mshtakiwa huyo Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray ametoa taarifa hiyo Leo Jumatano, Agosti 30, 2023 kupitia kwa wakili wake, Nehemiah Nkoko, kama Sheria inavyoelekeza.

Kwa mujibu wa kifungu Cha 194(4) na(5) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama mshtakiwa katika kesi ya jinai anakusudia kujitetea kuwa hakuwepo eneo la tukio kwa tarehe na wakati wa tukio husika anapaswa kwanza kuwasilisha mahakamani taarifa hiyo.

Aneth alikuwa mdogo wa aliyekuwa mfanyabiashara tajiri maarufu wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Agosti 7, 2013.

Aliuawa Mei 26, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo), jijini Dar es Salaam, na mwili wake ulikutwa ndani ya nyumba yake ukiwa uchi na nguo yake ya ndani ikiwa pembeni ya mwili huo.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 103/2018 inayosikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki ni Miriam Steven Mrita, ambaye ni mjane wa Bilionea Msuya, na mwenzake Muyalla.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Leo kabla ya mahakama hiyo kuanza kuendelea kupokea ushahidi wa shahidi wa 22, Wakili Nkoko anayemtetea mshtakiwa huyo wa pili aliieleza mahakama kuwa wamewasilisha mahakamani ilani ya mshtakiwa huyo kuwasilisha utetezi wa aina hiyo.

"Mheshimiwa Jaji jana tulifanikiwa kuwasilisha notice (taarifa) ya deffence ya alibi mtuhumiwa) mshtakiwa kutokuwepo eneo la tukio kwa siku au tarehe husika ya tukio husika) chini ya kifungu cha 194 (4), (5) cha (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai) CPA", amesema Wakili Nkoko na kuongeza:

"Kwa hiyo ifahamike kwamba mshtakiwa wa pili katika utetezi wake anakusudia kuwasilisha utetezi wa alibi."

Jaji Kakolaki amesema kuwa taarifa hiyo imepokelewa na kuwa sehemu ya mwenendo wa shauri hilo.

Baada ya maelezo hayo mahakama iliendelea kupokea ushahidi wa shahidi wa 22 wa upande wa mashtaka, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) David Paulo Mhanaya, ikiwa ni siku ya tatu leo kusimama kizimbani kutoa ushahidi wake.

Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kimweri shahidi huyo alieleza mahakama yale aliyoelezwa na aliyekuwa binti wa kazi wa marehemu Aneth; Getruda Peniel Mfuru, kuhusu matukio kabla ya mauaji ya mwajiri wake.

Aliieleza mahakama jinsi walivyoyafanyia kazi maelezo ya binti huyo wa kazi wa marehemu Aneth hadi wakawakamata washtakiwa jijini Arusha kwa nyakati tofauti na yale washtakiwa waliyoyaeleza baada ya kukamatwa na kuhojiwa

Leo, SSP Mhanaya, ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya upelelezi wa mauaji hayo iliyoteuliwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wa wakati huo, Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athuman, akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili Kimweri aliupinga utetezi aa m

Wakili Kimwei amemuongoza shahidi huyo aizungumzie ilani hiyo ya utetezi huo wa mshtakiwa wa pili alibainisha kuwa umeegemea katika simu zake tatu na maelezo yake ya onyo ambapo alikana tuhuma hizo, kuwa ndivyo vielelezo vya ushahidi wake kuonesha kwamba hakuwepo eneo la tukio.

Akizungumzia ilani hiyo na aina hiyo ya utetezi wa mshtakiwa huyo anaokusudia kuuwasilisha mahakamani, shahidi huyo ameema kuwa suala la simu kwanza siyo ushahidi unaoweza ukamuondoa mshtakiwa huyo kwenye shtaka hilo.

"Kwanza simu si sehemu ya mwili kwamba unakuwa umeibandika mwilini, mtu anaweza akaiacha sehemu akaenda kufanya uhalifu", amedai SSP Mhanaya na kuongeza:

'Ikumbukwe kwamba hawa walikuwa wamepanga kufanya uhalifu ndio maana wakatafuta simu ‘special’ (maalumu) wakampatia Getruda kwa ajili ya matumizi ya tukio hilo tu na ndio maana hata walimuambia kwamba baada ya mission (mpango) yao kukamilika simu hiyo ai-destroy (aiharibu) au aitupe mahali.ambako mtu mwingine hawezi kuipata."

Kuhusu maelezo yake ya onyo ambapo pia mshtakiwa huyo alikana kuwa hakuwepo eneo la tukio, shahidi huyo amedai kuwa haina mashiko.

"Hii pia ilikuwa haitoshi sisi kuamini mpaka tuendelee na upelelezi zaidi. Hivyo tulisikiliza aliyoyasema lakini sisi tuliendelea na upelelezi zaidi dhidi yake,” amedai shahidi huyo SSP Mhanaya na kuongeza:

"Ushahidi mwingine unaokinzana na mawazo ya mshtakiwa kuwa hakuwepo eneo la tukio kwanza tulipofika Dar es Salaam alitambuliwa kwenye gwaride la utambuzi na shahidi Getruda kwamba alikuwepo eneo la tukio pamoja na yule mama ambaye ni mshtakiwa wa kwanza."

Ameongeza; "Ushahidi mwingine pia mtuhumiwa sisi hatukumfahamu hivihivi alitajwa na mtuhumiwa (mshtakiwa) wa kwanza (Miriam) kwamba alipewa Sh20 milioni ili kutekeleza mauaji hayo ya kinyama."

SSP Mhanaya amedai kuwa ushahidi mwingine unaomuunganishjha mtuhumiwa na eneo la tukio ni kuwa na mwingiliano wa vinasaba na vielelezo vilivyokutwa eneo la tukio, baada ya sampuli za mpanguso wa mate kuchukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia

"Mheshimiwa Jaji kwa haya yote niliyoyaeleza na mkusanyiko wa uchunguzi uliofanyika utetezi wa mshtakiwa kwamba hakuwepo eneo la tukio hauna mashiko kabisa."

Maswali ya dodoso

Baada ya kuhitimisha ushahidi wake mkuu, akiongozwa na mwendesha.mashtaka, shahidi alihojiwa maswali ya dodoso na Wakili wa utetezi Peter Kibatala kuhusiana na ushahidi wake wote alioutoa kwa siku tatu, Kwa lengo la kuutikisa ili kuona uimara wake.

Sehemu ya mahojiano hayo ilikuwa kama ifuatavyo:

Kibatala: Umetoa hapa kielelezo P16 (kielelezo cha 16 cha upande wa mashtaka ambacho ni hati ya upekuzi kwa mshtakiwa wa pili, Muyella) mwambie Jaji hiyo ni Police form namba ngapi?

Shahidi: Ni upekuzi wa dharura

Kibatala: Ni Police form namba ngapi?

Shahidi: Ni Police form ya dharura

Kibatala: Namba ngapi?

Shahidi: Siko hapa kuizungumzia namba

Kibatala: Sasa huo ni ukorofi, angalia. PGO, 170, (Wakili Kibatala anampa shahidi Mwongozo wa Utendaji kazi wa Jeshi la Polisi akimuoneaha.mahali pa kusoma) kisha anamuuliza;   hiyo ni police form namba ngapi?

Shahidi: Usinilazimisha kujibu unavyotaka

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sasa namna hii hatutafika, naomba shahidi ajibu maswali kama ninavyomuuliza.

Jaji: Shahidi jibu swali

Kibatala: Soma hii PGO 170 ni form namba ngapi?

Shahidi: Anasoma kisha anasema; ipo kwenye CPA

Kibatala: Kabla ya kwenda kwenye CPA kwenye PGO 170 ipo au haipo?

Kibatala: Ambayo ni fomu gani?

Shahidi: Ni warrant register

Kibatala:  Ahaa kumbe hiyo ni warrant register, mimi nauliza maswali tu.... Sasa shahidi hiyo fomu unauyoiita warrant register ni wapi Jaji akisoma ataona kwamba upekuzi wa mshtakiwa wa pili ulifanyika Arusha

Shahidi: Nimeandika Olasiti, Olasiti iko Arusha Wakili Msomi usitake kunilazimisha uwe na heshima kama Wakili Msomi.

Kibatala: Shahidi, heshima ni nje huko, nimekuliza neno Arusha lipo?

Shahidi: Nimeandika Olasiti Kata ya Burka, iko Arusha

Kibatala: Mheshimiwa Jaji vinginevyo hatutafika tutakaa hapa mpaka.jumatatu Jumanne na hatutamaliza

Jaji: Shahidi jibu swali amekuuliza neno Arusha kama lipo?

Shahidi: Halipo

Kibatala: Shahidi pale juu umeandika anayefanyiwa upekuwzi ni Revocatus Everist Muyella, kweli si kweli?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Na ni kweli aliyesaini baada ya taratibu zote ni Revocatus Everist Mollel?

Shahidi: Ni mtuhumiwa

Kibatala: Shahidi kama ukitaka tukae hapa mpaka siku tatu nne niko tayari, Sisi tunataka tumalizw haraka urudi kwenye kutumikia majukumu yako. Nimekuliza aliyesaini ni Revocatus Everist Mollel?

Shahidi: Ni Revocatus Everist Muyella maarufu kama Ray

Kibatala: Ni kweli kwamba jina la Revocatus Everist Mollel umelipata kwenye cheti cha mafunzo ya mgambo?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Umesema kuwa mlikamata kitabu cha silaha, kineandikwa nani?

Shahidi: Kitabu cha silahankinaonwsha mmiliki ni Revocatus E P. Mollel wa box (sanduku la Posta) 605 Ilala Bomani

Kibatala: Shahidi ulisema umefundishwa na FBI, Unafahamu hiyo P ni kifupisho cha jina gani?

Shahidi: Sasa Mimi niitafute P...

Kibatala: Unaijua hiyo P ni ya jina gani?

Shahidi: Sijui

Kibatala: Uliieleza Mahakama kuhusu ushiriki wa hiyo bastola kwa mauaji?

Shahidi: Sikuieleza

Kibatala: Wewe ni mpelelezi mahsusi kabisa uliyeteuliwa baada ya wengine kuboronga Uliieleza Mahakama kuhusu hizo simu tatu milizozikamata relevance (uhusiano) yake katika kesi hii ni nini?

Shahidi: Tulizichukua kwa ajili ya uchunguzi

Kibatala:  Mkapata nini?

Shahidi: Hazikuwa na kitu nilisema walitumia simu maalumu ambayo walimwambia ai-destroy

Kibatala: Unafahamu Polisi linaruhusiwa kuiomba taarifa za mawasiliano ya simu?

Shàhidi: Nafahamu, zinafanywa na kitengo cha cybercrime (uhalifu wa kimtandao), mimi naizungumzia taarifa ambazo nimeshiriki kikamilifu

Kibatala: Mliwahi kuomba taarifa za simu za Revocatus Everist Muyella?

Shahidi: Jitihada zilifanyika lakini ilionekana watuhumiwa simu zao hazikutumika

Kibatala: Ulimwambia Jaji katika ushahidi wako kama namba za simu za mshtakiwa wa kwanza zilionekana zikiwasiliana na mshtakiwa wa pili?

Shahidi: Nilishasema taarifa hizo zitazungumziwa na mtaalam...

Kibatala: Wewe ulifanya?

Shahidi: Nimeshasema siwezi kuizungumzia

Jaji: Jibu wewe kama ulifanya?

Shahidi: Sikufanya Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Uliwahi kujua namba za simu za Getruda?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mliwahi kufahamu hiyo simu ilinunuliwa wapi?

Shahidi: Nimekwishasema hizo shughuli...

Kibatala: Nakuuliza wewe...

Shahidi: Sikufahamu

Kibatala: Shahidi ulisema uliiteuliwa na DCI nani vile?

Shahidi: Kamishna Diwani Athuma

Kibatala: Diwani Athumani Msuya?

Shahidi: Mi Sifahamu Nafahamu Kamishna Diwani Athuma, unainiwekea maneno mdomoni

Kibatala: Bila shaka hata hujui anatokea wapi?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na RCO Mchomvu (aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Temeke wakati huo) unamfahamu?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Sawa, hata waliokuteua huwafahamu. Ulisema baada ya kuteuliwa ulifanya kazj na RCO Mchomvu ni sahihi?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Kwa ufahamu wako wewe na timu yako pamoja na Mchomvu mlikuwa mnashughulikia jalada namba KGB/2849/2016?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Kwa hiyo ni dhahiri Mchomvu alikuwa analifahamu?

Shahidi: Kulifahamu vipi?

Kibatala: Kwa kuwa mlikuwa mnalifanyia kazi, uliwahi kufahamu kwamba kuna watuhumiwa waliwahi kukamatwa katika kesi hii?

Shahidi: Wakati huo hapakuwa na mtuhumiwa

Kibatala: Ni ushahidi wako chini ya kiapo kuwa huyu Getruda hakuwahi kukamatwa tarehe 27/5/2016 kwa tuhuma za mauaji ya Aneth Msuya?

Shahidi:Sio kweli, mimi Sifahamu

Kibatala: Haufahamu pia shahidi ofisa mpelelezi senior (Mwandamizi) kabisa kwamba boyfriend (mpenzi) wake Sabri Kombo aliwahi kukamatwa tarehe 27/5/2016 kwa tuhuma za mauaji ya Aneth?

Shahidi: Huyo alihojiwa kama shahidi.

Kibatala: Tarehe ngapi?

Shahidi: Ni muda mrefu siwezi kukumbuka, wewe unauliza umeshika karatasi na ni Wakili Msomi

Kibatala: Je ni tarehe 27/5/2016?

Shahidi: Siwezi kukumbuka

Kibatala: Unaifahamu hii taarifa? (Kibatala Anampatia shahidi huyo nyaraka moja akimtaka aitambue)

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nafurahi kwanza kwa Wakili kuniletea hii first crime report kwanza aithibitishie Mahakama yeye aliipata wapi maana hizi ni taarifa za ndani za Polisi na haiko kwenye committal proceedings ndio maana nimemwambia mimi naweza kuwa wakili lakini yeye hawezi kuwa Polisi.

Kibatala: Shahidi, Unafahamu au hufahamu ulichoshika ni kielelezo cha Mahakama na nimeomba kutoka mahakamani? Maana umeongea maneno meengi?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Unafahamu au hufanu ni kielelezo cha Mahakama na nimekuomba Mahakamani?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kwamba kimetolewa na Polisi mwenzako ambaye tulimlazimisha kuitoa hapa mahakamani?

Shahidi: Siwezi kuzungumzia ushahidi wa mtu mwingine.

Kibatala: Hufahamu halafu unazungumza maneno meeengi. Unafahamu kwa kujibu wa kielelezo hicho Getruda aliwahi kukamatwa tarehe 27/5/2016

Shahidi: Haiwezekani, hatuwezi kuongozwa kwa hisia

Kibatala: Kwa mujibu wa hicho kielelezo accused (mshtakiwa) anaitwa nani?

Shahidi: Anyway, accused anaitwa Getruda Peniel Mfuru( ananibu shahidi baada ya kuzungushana sana na Wakili mpaka Jaji akaingilia kati kumtaka ajibu kama alivyoukizwa.

Kibatala: Sehemu iliyoandikwa other accused ni nani?

Shahidi: Siwezi kuyasoma haya kwanza yamefutika

Kibatala: Authenticity (uhalisia) wanajua hawa mawakili, wewe soma jina la kwanza.

Shahidi: Sabri Haji Kombo Jaji,

Kibatala: La pili?

Shahidi: Wilbard Mathew Kimaro.

Kibatala: La tatu?

Shahidi: Amir (dereva bodaboda aliyewapakia Getruda na mpenzi wake Kombo siku ya tukio wakati akirejeaha funguo za geti la nyumba ya marehemu Aneth alizokuwa ameondoka nazo.

Kibatala: Shahidi kama mpelelezi uliyekwenda kuongeza nguvu, unafahamu huyo Mathew Kimaro alikuwa ni mume wa Aneth?

Shahidi: Najua

Kibatala: Unafahamu Aneth na huyo x mumewe walikuwa na ugomvi kuhusu mtoto?

Shahidi:

Kibatala: Baada ya kukuta karatasi chumbani kwa Aneth zimevurugwavurugwa uliwahi kuamuru huyo Kimaro ahojiwe?

Shahidi: Sikuwahi

Kibatala: Unafahamu huyo wa mwisho, Amiri ni bodaboda aliyewabeba Getruda na Kombo kuwarudiaha eneo la mauaji?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Uliwahi kutoa amri ahojiwe?

Shahidi: Alikuwa ameshahojiwa

Kibatala: Nakuuliza wewe ambaye uliteuliwa kwenda kuongeza nguvu kama uliamuru ili ahojiwe upya?

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Unafahamu marehemu kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa sababu za kifo alifariki saa Nne ?

Shahidi: Nafahamu alifanyiwa uchunguzi na Dk Chande

Jaji: Anauliza kama Unafahamu muda.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo pia hufahamu kuwa muda ule ambao Aneth alifariki ndio muda huo ambao yeye dereva bodaboda alikuwa amembeba Getruda na Kombo kwenda eneo la mauaji?

Shahidi: Sio kweli

Kibatala: Unafahamu au hufahamu?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mlipofika nyumbani kwa marehemu mkakuta milango imevunjwa uliwahi kufanya (uchunguzi wa alama za vidole) fingerprint?

Shahidi: Hayo yalishafanyika

Kibataka: Nakuuliza wewe?

Shahidi: Kulikuwa kumeshakuwa na muingiliano, hilo lisingeweza kufanyika maan kuna vitu vya kitaalamu ndio maana nakwambia wewe mimi naweza kuwa Wakili lakini wewe huwezi kuwa Polisi

Kibataka: Ulisema Aneth alikuwa na Filimbi, uliwahi kuuliza majirani kama wakati mlango umevunjwa aliwahi kupiga kuomba msaada?

Shahidi: Niliuliza kwa majirani lakini hawakusikia.

Kibatala: Unafahamu kwamba mpaka leo hii hufahamu majibu ya toxiology (taarifa kuhusu suala la sumu katika sampuli za marehemu zilizopelwkwa kufanyiwa uchunguzi) kwa Mkemia Mkuu?

Shahidi: Hilo suala la sumu halihusiani na tukio hili.

Jaji: Unafahamu?

Shahidi: Sifahamu mheshimiwa jaji na wala hilo halihusiani na tukio.

Kibatala: Ni kweli kwamba baada ya kifo cha marehemu Getruda alikimbia na hakutoa taarifa Polisi?

Shahidi: Alitoa taarifa kwa mpenzi wake Kombo

Kibatala: Kombo huyu ambaye naye alikamatwa Kwa tuhuma za mauaji ya Aneth. Alikuwa na umri gani ili kuona kama alikuwa amekomaa au la?

Shahidi: Sikumbuki?

Kibatala: Nini ambacho kitakukumbusha?

Shahidi: Nakumbuka tu alikuwa na watoto watatu.

Kibatala: Hii stori kuwa Getruda alipewa Sh50, 000 na Sabri Kombo (mpenzi wake) ulii-verify (uliithibitisha) vipi kama ni kweli?

Shahidi: Nili-verify kwa sababu alisafiri kwenda kwao Masama na alikamatwa huko ndipo akaletwa mimi nikafanya naye mahojiano.

Kibatala: Uliongea wewe au mmojawapo katika timu yako na Sabri mtoa nauli kuhusu hii Sh50, 000?

Shahidi: Aliongea naye ASP Jumanne

Kibatala: Aliongea naye specifically (maalumu) kuhusu hii nauli lini?

Shahidi: Atakuja kusema mwenyewe

Kibatala: Mheshimiwa Jaji...

Jaji: Shahidi, maelekezo yangu ni yaleyale jibu swali kama hukumbuki sema hukumbuki

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Ulimwambia Jaji alisafiri kwa gari gani?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Kwa mujibu wa hicho kielelezo (taarifa ya awali ya uhalifu ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji hayo)  Getruda alikamatwa tarehe ngapi?

Shahidi: Hii hapa naona 27 Mei 2016.

Kibatala: Sasa mwambie Jaji kwamba Getrud wakati anakuambia mambo mengi alikwambia alisafiri tarehe ngapi kwenda Moshi au Masama?

Shahidi: Mimi nilikabidhiwa tarehe 25/6/2016 nikafanya naye mahojiano kama nilivyosema.

Kibatala: Alikwambia ni lini alisafiri?

Shahidi: Ilikuwa tarehe 26/5/, Aliletwa tarehe 24..... Sikumbuki.

Jaji: Umelewa swali?

Shahidi: Sijaelewa

Kibatala: Getruda alikwambia aliondoka lini kwenda Masama baada ya kupewa nauli na mpenzi wake?

Shahidi: Tarehe 25/5/2016 ndo alikwenda kwake, Aliondoka tarehe 26/5/2016

Kibatala: Ni tarehe ngapi uli-form (ulijenga) opinion (maoni) ya kipelelezi kwamba Getruda si mshtakiwa ni shahidi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ilikuwa tarehe 26/8/2016

Kibatala: Wakati unamchukua Masama baada ya kuwatuma maafisa wako alikuwa (ametiwa mbaroni) under arrest or no?

Shahidi: Mimi Sifahamu Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Hawa subordinate (maafisa wadogo) wako uliowatuma waliripoti kwako kila walichokifanya Masama?

Shahidi: Kwanza nikusahihishe Msomi Wakili. Sikuwatuma mimi walitumwa na Afande Mchomvu.

Kibatala: Wakati anakabidhiwa kwako kwa mahojiano alikuwa katika hali gani, under arrest au?

Shahidi: Hakuwa under arrest.