Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi Banduka alivyoacha alama

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa, wakati wa uongozi wake, alikuwa na uwezo wa kujenga hoja, jambo lililomfanya akubalike na wenzake katika vikao mbalimbali vya wakuu wa mikoa

Mwanga. Viongozi wastaafu wameeleza mchango mkubwa alioutoa marehemu Nicodemus Banduka (80) katika Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa nyakati tofauti Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya na mkuu wa mkoa mstaafu, Daniel Ole Njoolay wamesema mwanasiasa huyo mkongwe alijulikana kwa uzalendo, weledi na uhodari wakati wa uongozi wake na alikuwa mfano wa kuigwa na wengine.

Banduka aliyewahi kushika nyadhifa ya ukuu wa Mkoa wa Ruvuma, Iringa, Shinyanga, Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa (NEC), alifariki dunia Februari 7, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mloganzila, jijini Dar es Salaam.

Banduka ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Mruma, Tarafa ya Ugweno, Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, amezikwa leo Jumatano Februari 12, 2025 katika makaburi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mruma, Dayosisi ya Mwanga.

Mkuu wa Mkoa mstaafu na Katibu wa Wakuu wa Mikoa Wastaafu, Ole Njoolay akitoa salamu za rambirambi, amesema Banduka alikuwa kiongozi mchapakazi na mfano wa kuigwa.

Amesema wakati wa uongozi wake, alikuwa na uwezo wa kujenga hoja, jambo lililomfanya akubalike na wenzake katika vikao mbalimbali vya wakuu wa mikoa.

"Banduka alikuwa mtu ambaye hoja zake ziliheshimika sana, alikuwa mbunifu na mchapakazi. Tumempoteza kiongozi wa mfano, jambo ambalo ni pigo kubwa kwetu," amesema Ole Njoolay.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu mstaafu, Msuya, Wakili Glider Kibola amesema Banduka ameacha alama ndani ya CCM, Serikali na jamii ya Mwanga kutokana na uchapakazi wake.

"Nimemfahamu Banduka kwa muda mrefu, tumefanya naye kazi katika shughuli za kijamii, ndani ya CCM na serikalini. Alikuwa kiongozi mwadilifu, mchapakazi na mwenye weledi mkubwa," ni ujumbe aliousoma Kibola kwa niaba ya Msuya.

Mtoto wa marehemu, Irene Banduka  akitoa historia ya baba yake, amesema kifo chake ni pigo kwa familia kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu.

Amesema mwaka 1968, Banduka alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kisha akaendelea na masomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  na mwaka 1971 alianza kazi kama mwalimu wa Sekondari ya Msalato.

Akitoa salamu za Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kada huyo  atakumbukwa kwa uzalendo wake na ni miongoni mwa walioshiriki kuhakikisha shule za sekondari za kata zinajengwa hapa nchini.

“Mzee Banduka amefanya kazi kubwa sana nchi hii, wakati ule tunajenga shule za sekondari za kata, alihakikisha zinajengwa, hata kipindi kile nikiwa DC (mkuu wa wilaya), alikuwa akipiga simu wewe DC nikija  Jumatatu nikute msingi umesimama na mimi niweke jiwe la msingi," amesimulia RC Babu.

Pia, amesema ni kiongozi ambaye muda wote alikuwa ni mcheshi na aliyeshirikiana na wenzake bila ubaguzi.

Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema Banduka atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka na uchapakazi wake wa mfano.
Nicodemus Banduka alijiunga na Tanu kati ya mwaka 1972 na 1976, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Tanu akiwakilisha vijana.

Pia, alikuwa miongoni mwa watu 20 walioteuliwa kuandika Katiba mpya ya CCM na aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa Kamati ya Kuandaa Katiba ya CCM.