Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jafo ataka uharaka usajili kampuni kuongeza ajira, kulinda haki bunifu

Waziri wa Viwanda na Biashara,Seleni  Jafo, akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni (Brela).

Muktasari:

  • Usajili huo utasaidia kuzalisha ajira nyingi hususani kwa vijana wanaohitimu vyuo.

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dk Selemani Jafo ametaka Wakala wa Usajili na wa Biashara na leseni (Brela) kuongeza kasi katika kusajili kampuni za watu binafsi, ili kuzalisha ajira nyingi hususani kwa vijana.

Jafo ametoa wito huo leo Jumatatu Septemba 9, 2024 alipotembela ofisi za Brela, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteliwa Julai 3, 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara.

Amesema amefurahiswa na taarifa kuwa kwa sasa kampuni kubwa zinasajiliwa ndani ya siku tatu, huku akibainisha kwa kampuni ndogondogo inahitajika uharaka zaidi ikiwezekana hata watu kujisajili kwa njia ya mtandao.

"Hakuna asiyejua kuna tatizo la ajira nchini kwetu na Serikali haiwezi kuajiri kila mtu, hivyo mnaposajili kampuni hizi mnaisadia Serikali kuondoa tatizo hilo.

"Mfano kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu na idadi inaongezeka kila mwaka na huenda kwa mwakani wahitimu zaidi ya 70,000 wakawepo mtaani.

"Hivyo, mnaposajili kampuni hizi mnasaidia pia vijana wetu kupata ajira au kujiajiri kwa wepesi," amesema waziri huyo.

Katika wito wake kwa watendaji wa wakala huo, amewataka kuwa na uhusiano mzuri miongoni mwao na taasisi nyingine wanazofanya nazo kazi na kuwasikiliza na kuwajali wafanyakazi wa chini.

"Jingine, naomba muwe wawazeshaji wa uanzishaji kampuni na biashara na si kugeuka kuwa kikwazo hata mahali ambapo mnaona kuna kanuni ambayo hata ikiachwa haiwezi kuleta athari au inaweza kufanywa hata kwa baadaye," amesema Jafo.

Pia ametaka wakala huo kuhakikisha wanalinda watu na haki bunifu zao, kwani kumekuwepo na malalamiko ya wabunifu kuibiwa kazi zao wakiwemo wasanii.

Awali, mwenyekiti wa bodi wa wakala huo, Profesa Neema Mori amesema kusajili kampuni ndani ya siku tatu ni moja ya mikakati waliojiwekea katika utendaji kazi wao.

Profesa Neema amesema ili kufanikisha hayo wamekuwa wakitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi wao, ili kufanya kazi kwa utaalamu zaidi na kujituma.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Godfrey Nyaisa amesema tangu walipoanza kuingiza taarifa katika mfumo wa kidigitali mwaka 2018 na kuhuisha nyingine, mpaka sasa wamesajili kampuni 205,507.

"Pia katika mfumo huo tumesajili majina ya biashara 561,014, alama za biashara 88248, Hataza 6275 na Viwanda 8074,” amesema.