Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Idadi ya watu waliofariki katika ajali Momba, yaongezeka

Songwe. Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya Tunduma imeongezeka na kufikia saba, huku wengine 14 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha Lori, daladala aina ya Hiace, pikipiki za matairi matatu na ‘bodaboda’ iliyotokea eneo la Mpakani wilayani Momba, Mkoa wa Songwe leo mchana.

Awali Kamanda wa Polisi mkoani hapa, ACP Theopista Mallya amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuwa watu 5 wamefariki na majeruhi 10

"Ajali hiyo ilitanguliwa na ajali ya daladala iliyogongana na Bajaji na kwamba wakati watu wakishangaa juu ya ajali hiyo kwenye mteremko, lori lililotoka Tunduma lilifeli breki na kuwasomba watu waliokuwa eneo la ajali ya awali," alisema Kamanda Mallya.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Tunduma, Dk Enock Mwambalaswa amesema katika ajali hiyo wamefariki watu saba na wengine 14 kujeruhiwa na kuwa majeruhi wamelazwa katika kituo hicho cha Afya cha Mpakani.

Mmoja wa shuhuda aliyekuwepo wakati tukio linatokea Francis Gideon amesema tukio la kwanza lilihusisha gari dogo lililokuwa likisafirishwa toka Dar es salaam kwenda nchi jirani lililoigonga pikipiki, lakini wakati watu wanasaidia kumuokoa dereva ndipo lilitokea lori ambalo lilikuwa linaelekea Mbeya likawapitia watu hao na kuyagonga magari mengine matatu.

"Nadhani Lori lile liliferi breki maana lilifika hapo kwa mwendo wa kasi na kuwagonga watu waliokuwa wakijaribu kumuokoa dereva wa bodaboda" alisema Gideon.