Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huzuni yatanda kwa Mbunge aliyefariki, wananchi wahofia miradi kuzorota

Waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbarali, Francis Mtega

Muktasari:

  • Mbunge huyo alifariki jana Julai 1 kwa ajali ya pikipiki 

Mbarali. Vilio na simanzi vimetawala nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Mbarali, Francis Mtega aliyefariki jana Jumamosi Julai 1, 2023 kwa ajali ya pikipiki akitokea shambani kwake.

Mwananchi Digital imefika nyumbani kwa marehemu na kushuhuhudia makundi mbalimbali ya watu yakiwa yamejitenga huku sura za huzuni zikiwa zimetawala na vikisikika.

Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Mbarali, Chama cha Mapinduzi (CCM)  pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Bahati Ndingo ni miongoni mwa waliofika nyumbani hapo kuwafariji familia, ndugu, jamaa na marafiki wa kiongozi huyo.

Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Wilaya ya Mbarami, Mathayo Mwangomo amesema limekuwa pigo kubwa kwa Jamii kuondokewa na kiongozi huyo aliyekuwa mpenda watu na maendeleo.

Amesema katika uhai wake alipenda kuwaunganisha wananchi lakini pia kushirikiana na jamii kwenye miradi ya maendeleo.

"Tutamkumbuka kwa mengi Mbunge wetu na moja ya ahadi zake ilikuwa kuunganisha wananchi kitu ambacho alifanikiwa, lakini kuchangia na kushiriki shughuli za maendeleo," amesema Mwangomo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Msalaka, Lufunyo Mwafute amesema miongoni mwa ahadi ambazo mbunge huyo aliahidi enzi za uhai wake ambazo zilikuwa hazijakamilika ni mradi mkubwa wa maji na shule ya sekondari Mwale ambayo ilikuwa haijaisha.

"Amefanya mambo mengi makubwa ikiwamo kituo cha afya na mengine tuna wasiwasi kama yataisha haraka kama mradi wa maji na ujenzi wa bweni kwenye shule ya sekondari Mwale,”amesema.

Taarifa za awali za familia zinasema Mtega atazikwa kijijini kwake Lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe Juni 5, 2023.