Haya ni mabadiliko mengine kwa manaibu Waziri

Muktasari:
- Mabadiliko mengine yafanyika kwenye Baraza la Mawaziri, Mnyeti ahamishiwa wizara ya uvuvi, Silinde aenda Kilimo.
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na uteuzi kwa manaibu waziri wawili.
Katika uhamisho huo aliyekuwa naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde, amepelekwa kutumikia nafasi hiyo katika Waziri ya Kilimo.
Silinde anachukua nafasi ya Alexander Mnyeti aliyedumu kwenye kiti hicho kwa saa chache tangu kuteuliwa akihamishiwa wizara ya mifugo na uvuvi.
Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeonyesha pia kufanyika kwa Balozi Aisha Amour kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi.
Sambamba na hilo Rais Samia amefanya uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mipango akiwemo
Wajumbe walioteuliwa ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela Omar Issa.
Wengine ni Balozi Mstaafu na Mjasiriamali Ami Ramadhan Mpungwe na Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Cambodia Maryam Salim.