Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Tulia uso kwa uso na Putin, wagusia mgogoro wa Ukraine

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson (kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Russia, Vladimir Putin (kushoto) jijini St. Petersburg.

Dar es Salaam. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Russia, Vladimir Putin jijini St. Petersburg nchini Urusi leo Ijumaa Julai 12, 2024.

Katika mazungumzo ya Dk Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania na Putin wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani duniani.

Kuhusu mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Spika Tulia amesema kabla ya kuzungumza naye tayari: “Tulishazungumza na maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie IPU itatengeneza fursa ya mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala.”


Endelea kufuatilia Mwananchi.