Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Tulia aboresha machinjio ya Mbeya, wafanyabiashara waeleza kilio chao

Dar es Saalam. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amelazimika kuchangia ujenzi wa miundombinu ya majengo kwenye machinjio ya ng'ombe eneo la Uyole ya Kati jijini Mbeya baada ya kukuta mazingira hatarisha   Kwa afya za walaji na wachunaji.

Dk Tulia ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini amefikia hatua hiyo leo Ijumaa Machi 24, 2023 ikiwa ni siku kadhaa baada ya kufanya ziara ya kukagua machinjio hiyo na kubaini kuwepo kwa mazingira machafu ya uendeshaji wa shughuli za uchinjaji wa mifugo hususani katika kipindi cha masika.

“Nilifika hapa hivi karibuni nimejionea hali ilikuwa ni mbaya sana hivyo nimelazimika kuboresha miundombinu ya majengo ikiwepo eneo la kuoshea nyama, jengo la kuchinjia na matenki ya kuhifadhia maji vyote vikiwa na thamani ya Sh3.2 milioni.

“Kwa kutambua afya ni mtaji kwasasa nina imani katika machinjio hii usalama wa nyama utakuwa bora zaidi tofauti na hapo awali kwani majengo yalikuwa yakivuja, eneo la kuoshea nyama hakuna na changamoto ya maji ilikuwa tatizo” amesema.

Dk Tulia mbali na kuchangia kuboresha miundombinu mbinu hiyo amesema ataendelea kuhakikisha huduma na mazingira rafiki zinaendelea kuboreshwa ili kuona watumiaji wa nyama na wachunaji wanakuwa salama.

Wakati huohuo amewawezesha mtaji wa Sh1 milioni kwa wakinamama wanaofanya biashara ndogondogo katika eneo hilo ili waweze kukuza mtaji ili kuweza kukuza uchumi wa kipato.

Kwa upande wake Ofisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Jiji la Mbeya, Amina Nalicho amesema kuwa wanakila sababu ya kumshukuru Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kwa kuboresha machinjio hiyo kwani ilikuwa na hali mbaya sana ya kiusalama ikiwepo ubora wa nyama kwa walaji.

“Hali ilikuwa mbaya sana kwani majengo ya kuchinjia mifugo, maeneo ya kuoshea na ukosefu wa huduma ya maji ilikuwa ikihatarisha usalama wa wachinjaji, mifugo na walaji" amesema Nalicho

Naye Mkaguzi wa ubora wa nyama Jiji la Mbeya, Pascal Mwihava amesema kwa siku wastani wa ng'ombe 18 mpaka 20 zinachinjwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo Mbunge amezitatua.

Mwenyekiti wa wafanyabishara wa machinjio hiyo,  Amani Mahenge ameomba Dk Tulia kuwasaidia kufikisha kilio chao kwa Jiji la Mbeya kuona umuhimu wa kujenga miundombinu ya uzio na eneo la kutunza uchafu.

Mkazi wa Uyole ya kati, Janeth Saimon amemshukuru Dk Tulia kwa kuboresha machinjio hiyo kwani awali walikuwa wakipata tabu ya kuwepo kwa harufu mbaya na mazalio ya nzi  iliyokuwa ikitokana na  uchafu kutokana na ukosefu wa huduma ya maji.