Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango awaonya wanafunzi CBE kuepuka anasa

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akitoa salamu za Mkoa kwa Makamu wa Rais Dk Philip Mpango leo alipofanya ziara kikazi mkoani Mbeya sambamba na kuzundua Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Dk Mpango leo Jumatatu, Julai 31, 2023 amezindua kuzindua miundombinu ya majengo katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya na kusisitiza maprofesa na walimu kutoa elimu itakayoketa matokeo chanya.

Mbeya. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameonya vijana wanaopata fursa ya elimu katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya kuepukana na anasa na badala yake chachu ya kibiashara za ndani na nje ya nchi.

Mpango amesema leo Jumatatu, Julai 31, 2023 baada kuzindua na kukagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Biashara sambamba na kuzungumza na wananchi wa Kata Iganzo jijini hapa.

“Nimekagua miundombinu ya majengo, niwaombe vijana mnaopata elimu, walimu kutunza rasirimali hiyo adimu na kuwashukuru wadau na wananchi waliochangia kuwepo kwa taasisi hii,” amesema.

Amesema anawashukuru wananchi waliotoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho kama tunavyofahamu biashara ni shughuli muhimu kwa maendeleo ya nchi licha ya kuwepo kwa changamoto ya wananchi kufanya biashara ya mazoea.

Dk Mpango amesema CBE kikawe chachu kuhakikisha vijana wanaopikwa katika kwenda kufanya biashara ya ushindani ndani na nje ya nchi.

Aidha Dk Mpango amemtaka Mkuu wa Mkoa, Juma Homera kwa kushirikiana na Spika wa Bunge ambaye ni mlezi wa Chuo  kuwa jicho la kuangalia uwekezaji wa elimu katika chuo hicho kwa vijana.

“Niwakaribishe kesho kushiriki katika kilele cha maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane kwenye Viwanja  John Mwakangale jijini Mbeya,” amesema.

Kwa Upande wake Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson amesema  wananchi na Wazee wa Kata ya Iganzo walitoa eneo lenye ukubwa wa ekari 54 kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.

“Makamu wa Rais, wazee wa eneo hili walitoa eneo licha ya wengine kulipwa fidia ni jambo la kuwashukuru pia tufikishie salamu kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tumepokea Sh1 bilioni kwa ajili ya mradi wa maji.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema mkoa umetoa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha madaktari bingwa ili kuongeza fursa kwa vijana.

Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho, Prof Wineaster Anderson amesema mradi huo umegharimu zaidi ya Sh1.4 bilioni kati ya hizo Sh350 milioni ni fedha kutoka Serikali Kuu.

Amesema kwa kipindi cha miaka iliyopita chuo hicho kilifanya mafunzo kwa wafanyabishara na wajasiriamali 600 kutoka mikoa ya Dodoma, Mwanza na Mbeya.

Amesema kwa awamu hii ya kwanza chuo kimedaili wanafunzi 12,000 na matarajio ni kuongeza idadi na kufikia 20,000.