Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango akemea unyonyaji, rushwa kumuenzi Mwalimu Nyerere

Rais Samia Suluhu Hassan akifurahi jambo na Makamu wake, Dk Philip Mpango atika misa ya kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu mjini Babati mkoani Manyara.

Muktasari:

  • Dk Philp Mpango ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo kupinga vita vya unyonyaji na ukandamiza, vitendo vya rushwa na ufisadi akisema ndio njia bora ya kumuenzi mwasisi wa Taifa hili, Hayati Julius Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999 jijini London Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amesisitiza kulinda Uhuru wa Taifa, kupinga unyonyaji na ukandamizaji ni namna ya bora kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

 Dk Mpango ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 14, 2023 katika misa ya kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu mjini Babati mkoani Manyara.

Misa iliyoongozwa na Askofu Jimbo Katoliki la Mbulu, Anthony Lagwen ilihudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Oktoba 14 ya kila mwaka Taifa linafanya kumbukizi ya kifo cha Mwalimu Nyerere, aliyekuwa rais kwa kwanza aliyefariki dunia tarehe na mwezi kama huu 1999 jijini London, Uingereza katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas.

“Tukumbuke wajibu wetu, katika Taifa letu ndio namna bora zaidi ya kumuenzi Mwalimu Nyerere, kubwa zaidi kulinda Uhuru wa Taifa, kukataa aina yoyote ya unyonyaji na ukandamizaji,” amesema Dk Mpango.

Dk Mpango ameendelea kwa kusema kuwa Nyerere aliamini katika usawa, aliwaona binadamu wote kuwa ndugu zake, hivyo Watanzania wanapaswa kuyaishi hayo.

Amesema Nyerere alichukia rushwa, hakuvumilia vitendo vyovyote vya harufu ya rushwa wala ufisadi ni wajibu kwa Watanzania kuyaishi hayo pia.

“Alithamini dhamana aliyopewa, hakutumia cheo chake kwa faida yake Makongoro upo hapa (mtoto wa Nyerere), hata ile nyumba nzuri ya Butiama alikuja kujengewa na Serikali.

Dk Mpango amewataka viongozi wa Serikali kujitakafari hasa wale wanaojilimbikizia mali kwa kutumia vibaya nafasi zao sio njia njema ya kumuenzi Mwalimu Nyerere.

Akiwasilisha salamu hizo, kwa niaba ya Rais Samia, kiongozi huyo amesema Nyerere alitumia elimu na vipaji alivyopewa kupiga vita umasikini na alikuwa mnyenyekevu, hakusita kujisahisha pale alipobaini amekosea.

“Sisi viongozi wa wananchi pale ambapo tunakosea, tukiri kama tumekosea ili kujisahisha. Nyerere alikuwa mwadilifu hakupenda kutumia mali za umma kujinufaisha, alikuwa mlinzi wa mali za umma.

“Alijenga na kuimarisha maadili katika jamii, hakusita kukemea matendo mabaya yaliyochochea mmonyoko wa maadili. Alipenda mazingira, alikuwa mkulima hodari, tumuenzi kwa kuendelea kwa kuchapa kazi kwa bidii ili kujipatia kipato,” amesema Dk Mpango.

Katika hatua nyingine, Dk Mpango amesema Rais Samia ametoa Sh100 milioni kwa ajili ya kubariki kanisa hilo, lililotimiza miaka 10 tangu kujengwa, shughuli itakayofanyika mwaka 2024.

Akiwa katika harakati za kutoa mchango wake, baada ya kumtaka alichokitoa Rais Samia, Dk Mpango alisema yeye atachangia lakini sio kama alivyoahidi bosi wake (Rais Samia) ili kufanikisha shehere hizo.

Lakini kabla ya kufikia hatua alionekana akifanya mawasiliano na Rais Samia aliyekuwa ameketi viti vya mbele, ambaye alimwambia kuwa kati ya Sh 100milioni, Sh50 milioni amemtolea yeye.

“Bosi wangu (Rais Samia) ananipenda kumbe katika ile 100 (Sh100 milioni) nusu ananitolea mimi msaidizi wake,”amesema Dk Mpango na kupigiwa makofi na waumini waliohudhuria misa hiyo.

Awali Askofu, Lagwen amesema Mwalimu Nyerere alipigania Uhuru wa Tanganyika, lakini pia ni Rais wa kwanza wa Taifa hili, alikuwa mcha Mungu.

Amesema Nyerere alishiriki kwa kiwango kikubwa kujenga misingi ya usawa, haki, amani, umoja na mshikamano. Pia ameshiriki katika jitihada za ukombozi katika mataifa mbalimbali.

“Alikuwa kiongozi mpatanishi ndani ya nchi na nje, pia alikuwwa mzalendo. Tunapofanya kumbukizi, basi tunamshukuru Mungu kwa sabbau tulipata bahati ya kulelewa na kuishi na mtu aliyekuwa mcha Mungu,” amesema Askofu Lagwen.