Dk Biteko: Ushirikiano nchi za Afrika utasidia upatikanaji nishati ya kutosha

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko
Muktasari:
- Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko, amesema licha ya Afrika kuwa na utajiri wa aina mbalimbali za rasilimali za nishati ikiwemo nishati jadidifu, viwango vya upatikanaji wa nishati barani Afrika bado viko chini ikilinganishwa na mataifa mengine.
Unguja. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko, amesema licha ya Afrika kuwa na utajiri wa aina mbalimbali za rasilimali za nishati ikiwemo nishati jadidifu, viwango vya upatikanaji wa nishati barani Afrika bado viko chini ikilinganishwa na mataifa mengine.
Dk Biteko alitoa kauli hiyo leo Septemba 15, 2023 alipomwakilisha Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, kufungua mkutano wa kikao cha kamati maalumu ya kiufundi ya uchukuzi, miundombinu ya Tehama na nishati kwa nchi za Umoja wa Afrika (AU), kilichofanyika Zanzibar.
Kikao hicho kilitanguliwa na vikao vya kiutendaji na kuzindua ripoti ya Mpango wa Maendeleo ya Miundombinu Barani Afrika ya miaka 10 (Pida).
Dk Biteko amesema kuna umuhimu nchi za Afrika kukabiliana na upungufu huo na kwamba lazima uchukuliwe kwa uzito unaostahili kufanya kazi kwa pamoja kama nchi wanachama kutumia fursa hizo kuwekeza ili Afrika ziwe kunufaika na huduma za nishati.
“Tunaipongeza kamisheni ya Afrika na Shirika la Maendeleo la Afrika kutengeneza soko moja la umeme la Afrika na mpango Mkuu wa umeme wa ndani juhudi hizi zinathibitisha zitatusaidia kuunganisha mtandao wa meme Afrika katika kufanya kazi ya kuongeza uwepo wa nishati hiyo Afrika,” amesema
Amesema hatua hiyo itaongeza ushirikiano na kutoa ajira kwa wananchi hususani vijana na kukuza ushindani wa Afrika kwa ujumla.
Hata hivyo amesema Tanzania ina miradi mikubwa ambayo imeweza kuungaisha gridi zake pamoja na nchi jirani za Burundi na Rwanda huku kukiwa na mradi mwingine utakaounganisha Tanzania na Kenya ikiwa upo mwishoni kukamilika.
“Hatua hiyo itawezesha kuunganisha gridi ya Ethiopia kupitia Kenya, pia itaunganisha gridi ya Tanzania na Zambia mradi utakaounganisha pia Kusini mwa Afrika, pia Tanzania na Malawi zimesaini makubaliano kwa ajili ya kuzalisha ueem wa songwe wenye uwezo wa kuzalisha megawati 180.2,”amesema
Pia amesema Tanzania inaendelea kutekeleza miradi mingine ya kimkakati katika sekta ya uchukuzi ili kuifungua kiuchumi ukiwemo ujenzi wa reli ya kisasa yenye urefu wa kilometa 1800 huku ikiendelea kuweka kipaumbele katika nishati kwa kujenga bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa kilometa 1400
Upande wa uchukuzi imeboresha shirika la ndege kwa kuwa na ndege 12 zinazoiunganisha na mataifa mengine.
Akizungumza kuhusu ripoti iliyozinduliwa kuhusu utekelezaji wa miradi ya katika sekta hizo Afrika, Kamishna wa miundombinu na nishati wa AU, Dk Amani Abou-Zeid amesema kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa taarifa baina ya nchi na nchi.
“Tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja na kushirkiana kuhakikisha taarifa zinapatikna, kila nchi inatekelza miradi yake lakini inapokuja sula la upatikanaji taarifa vinginevyo hatutakwenda popote,”
Pia amesema ni vyema kuzishirikisha sekta binafsi ili kuwa an mawazo, na juzi mpya katika utekezaji wa miradi hiyo.
Naye Makamu Mkuu wa Rais wa Afrika Mashariki ya kati ya Shirika la Uwakala wa Kimataifa la Japan (Jica), Ando Naoki amesema shirika hilo litaendelea kushirika na kuzisaidia nchi za Afrika katika mipango yake ya maendeleo
Naye Mkurugenzi wa Miundombinu, Biashara na Viwanda Mtangamano wa kikanda AU, Amine Idriss amesema wanapaswa kuchangia katika uwajibikaji ili kuleta mabadiliko.
Umeonyesha jinsi ambavyo wanaweza kutekeleza miradi mingi ambayo inaleta matokeo chanya kwa bara la Afrika na wananchi kupata umeme kwa zaidi ya watu 20 milioni.