Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Biteko aeleza Afrika inavyoweza kuongeza upatikanaji wa umeme

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko akizungumza wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa nishati unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika, mashirika ya kimataifa; viongozi wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na taasisi ya Rockefeller (M300) inayofanyika leo Jumatatu, Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Inakadiriwa kuwa waafrika milioni 571 bado hawajafikiwa na nishati ya umeme, licha ya jitihada zilizofanywa ndani ya Bara la Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa umeme, huku jitihada za pamoja zikihitajika

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Doto Biteko amesema ni wakati wa kutumia fursa zote za nishati zinazopatikana katika Bara la Afrika ili kusaidia kuondoa upungufu wa nishati uliopo.

Dk Biteko amesema, pamoja na jitihada zilizofanywa katika nchi za Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa nishati, inakadiriwa kuwa Waafrika milioni 571 bado hawana umeme.

Amesema hayo leo Jumatatu, Januari 27, 2025 wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika kongamano la nishati barani Afrika linalolenga kutoka na maazimio yatakayowezesha Waafrika milioni 300 kufikishiwa huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030.

Dk Biteko amesema zimepita zama ambapo umeme ulikuwa ulionekana kuwa bidhaa ya ziada, lakini sasa ni bidhaa ya msingi inayohitajika kwa ajili ya maendeleo.

“Ni wakati wa kutumia fursa zote za nishati katika Bara la Afrika na kuondoa upungufu wa nishati uliopo. Tutumie mkutano huu kuja na mkakati utakaolenga kutekeleza malengo ya nishati ili kuimarisha ushirikiano unaohitaji kama bara,” amesema.

Amesema baada ya uhuru katika miaka ya 1960, nchi za Afrika zimepiga hatua kubwa katika kuzalisha na kusambaza umeme kwa wananchi wao, akitoa mfano wa Tanzania ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa na megawati 21 na leo inazalisha megawati zaidi ya  3,100.

“Mwishoni mwa mwaka huu uwezo wa nchi katika uzalishaji wa nishati utafikia megawati 4,000 na asilimia 61 itatoka katika nishati safi ambayo itawanufaisha wakazi wa mijini na vijiji na hadi sasa vijiji 12,000 vimeshafikiwa na umeme,” amesema.

Katika mtengamano wa Afrika mtandao wa umeme wa Tanzania umeunganishwa na Rwanda, Kenya Burundi na Uganda na njia nyingine zinatengenezwa kwa ajili kuuganishwa na Zanzibar.

Katika kufanikisha hilo, Dk Biteko amesema uwekezaji zaidi unahitajika katika sekta ya nishati, kwani ina nafasi ya kukuza sekta ya viwanda, madini na hoteli, hali inayohitaji uwekezaji wa kimkakati ili kufikia mahitaji ya siku zote.