Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diwani Mbozi asimamishwa hadi Januari 2025 kwa utovu wa nidhamu

Diwani wa kata ya Isalalo katika habari picha aliyesimmishwa kuhudhuria vikao katika halamashauri ya Mbozi. Picha na Denis Sinkonde

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, George Musyani Musyani amedai kuwa diwani huyo amekuwa akitumia cheo chake vibaya kwa kufanya makosa ya utovu wa nidhamu na kudhalilisha cheo cha udiwani.

Mbozi. Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mbozi Mkoani Songwe limemsimamisha kuhudhuria kikao kimoja cha baraza hilo Diwani wa Kata ya Isalalo, Baraka Haonga kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na kudhalilisha cheo cha udiwani.

Mbali na kutohudhuria kikao hicho kinachotarajia kufanyika mwezi huu, diwani huyo pia ametakiwa kutojihusisha na shughuli za udiwani hadi Januari 2025 baraza hilo litakapokutana tena.

Uamuzi wa baraza hilo umetangazwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, George Musyani wakati wa kikao cha robo ya pili jana, baada ya ajenda za kiutumishi na kwa kauli moja madiwani wakaridhia kumsimamisha.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi leo hakuweka wazi a utovu wa nidhamu aliofanya diwani huyo na kusisitiza ameitwa mara kadhaa kuonywa, lakini amekuwa akifanya makosa ya kujirudia.

"Tumemwita mara tatu kwenye vikao vya nidhamu na kumuonya mara kadhaa juu ya mwenendo wake na kikao cha mwisho ameitwa Oktoba, 2024 lakini bado anaendelea na tabia ya utovu wa nidhamu.

"Itoshe tu kusema diwani huyu amesimamishwa kwa sababu ya utovu wa nidhamu, hivyo asubiri adhabu yake iishe ndipo ataendelea na majukumu ya vikao vya madiwani na shughuli za udiwani kwenye kata yake ya Isalalo," amesisitiza Musyani.

Akizungumza na Mwananchi Diwani Haonga amesema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote juu ya uamuzi huo, kwani ameacha uchunguzi wa jambo hilo ufanyike juu ya tuhuma anazokabiliana nazo ndipo atazungumza.

Si mara ya kwanza Kwa halmashauri hiyo kumsimamisha diwani kuhudhuria vikao, kwani mwaka 2018 baraza hilo lilimsimamisha vikao vitatu Diwani wa Kata ya Ipunga, Wilaya ya Mbozi, Bartoni Sinienga.