Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva teksi akamatwa akituhumiwa kumuua abiria miaka tisa iliyopita

Ulumbi Stephano (62) mwenye ulemavu wa miguu enzi za uhai wake

Muktasari:

  • Baada ya kutafutwa kwa miaka tisa, Polisi mkoani Morogoro wamemkamata Omari Mwanamtwa (60), dereva wa taksi anayetuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Ulumbi Stephano aliyekuwa  na ulemavu wa miguu.

Morogoro. Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Omari Mwanamtwa (60), dereva taksi, mkazi wa Chamwino Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kumuua abiria wake Ulumbi Stephano (62) aliyekuwa na ulemavu wa miguu.

Mwanamtwa anadaiwa baada ya kufanya mauaji hayo miaka tisa iliyopita alitoroka.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama amewaeleza waandishi wa habari leo Alhamisi, Machi 6, 2025 kuwa tukio hilo la maujaji lilitokea Machi 2016 katika eneo la Kasanga, Manispaa ya Morogoro na mpaka sasa mwili wa marehemu haujapatikana.

"Huyu mama mwenye ulemavu ambaye enzi ya uhai wake muda mwingi alikuwa akitumia teksi ya mtuhumiwa, ghafla alipotea na baada ya uchunguzi wa polisi teksi hiyo ilikutwa imetelekezwa kwenye kituo kimoja cha mafuta ikiwa na damu.

Kutokana na hali hiyo, uchunguzi wa kitaalamu uliofanyika ulibaini damu iliyokutwa kwenye ile teksi ilikuwa ya Ulumbi Stephano,” amesema.

Kamanda huyo amesema teksi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa, ni mali ya Mayasa Hashimu, ofisa elimu mstaafu na mkazi wa Tanga.

Amesema kwa sasa mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na uchunguzi wa polisi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Akizungumzia namna mtuhumiwa huyo alivyokamatwa, Kamanda Mkama amesema ni baada ya kupenyezewa taarifa kutoka kwa raia wema wanaofahamu tukio hilo, ambao walimuona nyumbani kwake na baada ya taarifa hizo polisi waliweka mtego na kumkamata.

"Hili tukio lilitikisa hapa Morogoro na huyu jamaa tayari tulishatangaza kuwa tunamtafuta, hivyo aliporudi tu nyumbani kwake watu wakatueleza na sisi tukafanyia kazi taarifa hizo, hatimaye tukafanikiwa kumkamata," amesema Kamanda Mkama.