Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DCEA yabaini mbinu mpya kusafirisha dawa za kulevya kupitia fuvu la maiti

Muktasari:

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema imebaini mbinu ya kusafirisha dawa za kulevya inayotumiwa na baadhi ya wahalifu kupitia maiti za binadamu maarufu kwa jina la 'begi'.


Dar es Salaam. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema imebaini mbinu ya kusafirisha dawa za kulevya inayotumiwa na baadhi ya wahalifu kupitia maiti za binadamu maarufu kwa jina la 'begi'.

Akizungumza leo Julai 9, 2025 katika ofisi zilizopo Kivukoni Dar es Salaam, Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo amesema wahalifu wanatoa fuvu la kichwa halafu wanatoa Ubongo kisha wanaweka dawa hizo.

"Tumeshakamata baadhi ya maiti tumezifanyia uchunguzi tumebaini, wahalifu hao wanapasua utumbo, kifua, wanatoa utumbo, maini kisha wanajaza dawa hizo," amesema.

"Mwanzoni walikuwa wanapasua tumbo wanajaza lakini hivi sasa wanapasua kifua kwenye mapafu pale wanaondoa na maini halafu wanajaza kwa hiyo usipoangalia kwa umakini unaweza usigundue," amesema Kamishna Jenerali huyo.

Ameomba wananchi kuwa makini wanaposafirisha maiti zinazotoka ughaibuni kuja nchini kwa sababu zikitumika kubeba dawa za kulevya wakibainika na wao wanaingia hatiani.

Aidha, Kamishna Jenerali huyo amesema hata wale wanaomeza dawa hizo kupita katika viwanja vya ndege sasa hawataweza kutokana na mifumo iliyopo hivi sasa.