Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DAS Ileje atoa miezi miwili kila kaya kuwa na choo bora

Katibu Tawala wilaya ya Ileje Abdala Mayomba akizungumza wakati wa kikao Cha afya ya msingi kikichoandaliwa na shirika la EEPCO kwa lengo la kujadili ujenzi na matumizi ya vyoo bora. Picha na Denis Sinkonde

Muktasari:

  • Mayomba ametoa miezi miwili kwa watendaji wa kata kuhakikisha wanafuatilia kaya zote ambazo bado hazina vyoo bora ili ndani ya kipindi hicho kaya zote katika wilaya hiyo ziwe zimeboresha huduma za usafi wa mazingira.

Ileje. Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe inatarajia kuanza kutekeleza sheria na kanuni zitakazolenga kuhamasisha wananchi kujenga na kutumia vyoo bora ili kulinda afya za jamii na kupunguza magonjwa yanayosababishwa na mazingira duni ya usafi.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ileje, Abdallah Mayomba wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri uliopo Itumba leo Juni 5, 2026 kikiwa kimeratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la EEPCO ambalo linafanya kazi ya kuhamasisha wananchi kujenga vyoo bora katika vijiji 40 ndani ya kata 12 kati ya 71 wilayani humo.

Mayomba amesema miongoni mwa sheria zitakazochukuliwa kwa wananchi watakaokosa vyoo bora ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kulingana na sheria za afya ya mazingira ikiwepo kukamatwa na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria ndogondogo zilizotungwa na halmashauri.

Amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Nuru Kindamba kukamilisha utaratibu wa matumizi ya sheria ndogo za halmashauri ili kuimarisha usimamizi wa afua za usafi na mazingira.

Mayomba ametoa miezi miwili kwa watendaji wa kata kuhakikisha wanafuatilia kaya zote ambazo bado hazina vyoo bora ili ndani ya kipindi hicho kaya zote katika wilaya hiyo ziwe zimeboresha huduma za usafi wa mazingira.

Katibu Tawala huyo amebainisha hatua hizo muda mfupi baada ya mwakilishi kutoka shirika la EEPCO, Robius Bagoka kubainisha takwimu ya hali ya matumizi na ujenzi wa vyoo bora katika vijiji 40 wilayani humo.

Bagoka amesema katika kipindi cha Januari hadi Machi 2026 asilimia 59.50 ya kaya 11,087 zina vyoo bora kati ya kaya 18,636, asilima 39.23 ya kaya 7,311 bado zinatumia vyoo vya asili na asilimia 0.82 ya kaya 152 hazina vyoo kabisa.

Amesema shughuli hiyo ya utambuzi wa vyoo bora kwenye kaya imeenda sambamba na kubaini kaya zenye vyombo vya kunawia mikono ambapo kaya 8,615 kati ya kaya 18,636, sawa na asilimia 46.24, zina vifaa vya kunawia huku idadi ya kaya nyingi zikiwa hazina vifaa hivyo.

Bagoka amesema baadhi ya ofisi za Serikali ikiwepo ofisi za vitongozi, vijiji, kata, shule pamoja na makanisa, sehemu za vilabu za pombe za kienyeji mashine za kusaga hazina vyoo bora pamoja na milango kitendo ambacho kinaweza kuleta ugumu kwa wananchi kutekeleza takwa la kisheria la ujenzi wa vyoo kwenye kaya zao.

“Wakati tunaanza kutekeleza mradi huu Oktoba – Desemba 2025, asilimia 51 ya kaya zilikuwa na vyoo bora, asilimia 45 zilikuwa na vyoo vya asili na asilimia 1 kaya hazikuwa na vyoo kabisa,” amesema Bagoka.

Akizungumzia kuhusu hali ya matumizi ya vyoo bora, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Ileje, Nuru Kindamba amesema kabla ya mradi wa ujenzi wa vyoo na usafi wa mazingira kupitia EEPCO, halmashauri hiyo ilikuwa na hali mbaya ya vyoo kutokana na mila na desturi zilizokuwa zikiwataka watoto kutotumia choo kimoja na wazazi wao.

Kindamba amesema kupitia mradi huo umesaidia kuelimisha jamii kuanza kujenga vyoo bora, kitendo ambacho takwimu za mradi ulivyoanza na sasa kuna mabadiliko, hivyo Halmashauri ya Ileje ni mfano bora wa ujenzi na matumizi ya vyoo bora.

Mwezeshaji kutoka shirika la EEPCO Robius Bagoka akiwaasilisha taarifa ya Hali ya vyoo bora katika kata 12 wilayani Ileje mkoani Songwe ambako shirika hilo linatekeleza mradi. Picha na Denis Sinkonde

Amesema licha ya kampeni mbalimbali za uhamasishaji kufanyika kwa miaka mingi, bado baadhi ya wananchi wamekuwa wakisuasua kujenga vyoo bora, jambo linalochangia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko yakiwamo kipindupindu na kuhara.

“Lengo si kuwaadhibu wananchi, bali kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo salama kinacholinda afya ya familia na jamii kwa ujumla,” amesema Kindamba.

Harsoni Chanya, mkazi wa Itumba, akizungumza kwenye kikao hicho, amesema Serikali kupitia wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu pamoja na kuwawezesha upatikanaji vifaa vya ujenzi wa vyoo bora kwa gharama nafuu ikiwepo vyoo vya aina ya sato.

Chanya amesema kulipishwa faini kwa wananchi watakaokaidi utekelezaji wa ujenzi wa choo bora itasaidia kuongeza uwajibikaji katika suala la usafi wa mazingira.