Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yazindua kadi mpya za kielektroniki

Katibu mkuu wa CCM,  Daniel Chongolo akimkabidhi mwemyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan kadi ya mfano ya kielektroniki baada ya mwenyekiti huyo kuzindua kadi hizo mjini Musoma kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM

Muktasari:

  • Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kadi mpya za wanachama za kielektroniki zenye taarifa na kumbukumbu muhimu za mwanachama zitakazowatambulisha na kuwawezesha kupata huduma za kifedha.


Mwanza. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kadi mpya za wanachama za kielektroniki zenye taarifa na kumbukumbu muhimu za mwanachama zitakazowatambulisha na kuwawezesha kupata huduma za kifedha.

Uzinduzi wa kadi hizo umefanyika mjini Musoma leo Jumamosi Februari 5 ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho tawala kilichoundwa Februari 5, 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya ukombozi vya Tanu (Tanganyika) na Afro Shirazi kwa upande wa Zanzibar.

Kadi hizo zimezinduliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia amekabidhiwa kadi ya kwanza na Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuzinduliwa kwa kadi hizo Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema kupitia kadi hizo  wanachama wa CCM zaidi ya 12 milioni siyo tu watatambulika kirahisi, bali pia wataweza kutumia kadi zao kupata huduma za kifedha.

Katibu mkuu wwa CCM,  Daniel Chongolo akimkabidhi kadi ya kielektroniki mwenyekiti wa chama hicho,  Samia Suluhu Hassan baada ya mwenyekiti huyo kuzindua kadi za CCM za kielektroniki

Kwa mujibu wa Chongolo, wanachama zaidi ya 2.07 milioni tayari wamesajiliwa kupitia huo mfumo mpya wa kielektroniki.

Kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM zinazohudhuriwa na zaidi ya wageni 5, 000 kutoka ndani na nje ya nchi zinafanyika uwanja wa kumbukumbu wa Karume mjini Musoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyezaliwa mwaka 1922.

Hii ni mara ya pili kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM kufanyika katika uwanja huo ambapo kwa mara ya kwanza shughuli hiyo ilifanyika hapo mwaka 1985 yakiongozwa na Rais wa Tanzania wakati huo, Ali Hassan Mwinyi.

Ujio wa ugeni huo umeufanya mji wa Musoma na vitongoji vyake kujaa shamrashamra huku mitaa yote imepambwa kwa bendera na kila aina ya mapambo yenye rangi zinazowakilisha CCM pamoja na picha za Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho tawala.

Viongozi wengine wa Kitaifa wanahudhuria sherehe hizo zilizopambwa kwa burudani mbalimbali kutoka kwa vijana wa chipukizi na vikundi vya Sanaa ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk Hussein Ali Mwinyi, makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Kassim majaliwa, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.


Kabla ya kufikia kilele leo, maadhimisho hayo yalitanguliwa na ziara za viongozi wa Kitaifa wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu, Daniel Chongolo waliotembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote sita za mkoa wa Mara.


Viongozi wengine wa CCM waliofanya ziara na wilaya walizotembelea kwenye mabano ni Katibu mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Kenani Kihongosi (Tarime na Rorya), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT), Gaudencia Kabaka (Butiama), Katibu NEC, Siasa na Uchumi, Ngemela Lubinga (Musoma) na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Christina Mdeme alyetembelea Wilaya ya  Serengeti.