Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yawalilia waliopoteza maisha ajalini Njombe

Muktasari:

  • Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetuma salamu za rambirambi kwa familia za viongozi sita wa chama hicho waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea Oktoba 13 mwaka huu katika eneo la Ndulamo Wilaya ya Makete mkoa wa Njombe.

Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetuma salamu za pole na rambirambi kwa familia zilizopoteza ndugu zao sita katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ndulamo, wilayani Makete, Mkoa wa Njombe.

 Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambao pia walikuwa viongozi wa chama hicho ni Hebron Mbilinzi ambaye ni Katibu wa CCM, Kata ya Tandala, Tumaini Mbilinyi (Katibu Mwenezi Kata ya Tandala), Linus Sanga (Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Ihela – Tandala).

Wengine ni Ruth Sanga (Mwenyekiti wa UWT Kata Lupila), Speransia Sanga (Katibu wa UWT Kata Maliwa – Ipepo) na Eva Sanga (Katibu UWT Kata ya Lupila).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho, Sophia Mjema leo Oktoba 14, 2023; inaeleza kuwa uongozi wa chama unatoa pole kwa familia hizo.

“Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan, unatoa salamu za pole kwa familia za marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Vifo hivyo vilisababishwa na ajali ya gari iliyotokea Ijumaa ya Oktoba 13, 2023 ikihusisha gari aina ya Toyota Hiace iliyokuwa imewabeba viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka kutekeleza majukumu ya chama ya katika ziara ya Mlezi wa Mkoa huo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Imori alipothibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana, amesema ilitokea saa 11 za jioni katika eneo lenye kona kali iliyopo Kijiji cha Ndulamo.

Kamnda Imori amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo n ini mwendo kasi ambapo inadaiwa gari hiyo iliyokuwa ikitokea Wilaya ya Makete kwenda Tandala, ilipofika kwenye eneo hilo, dereva alishindwa kuidhibiti, ndipo lilipinduka na kusababisha vifo vya watu sita pamoja majeruhi.

"Gari hiyo ilibeba abiria 18, kati ya hao sita wamepoteza maisha huku maieruhi 11 wamekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi, chanzo cha ajali ni mwendo kasi na dereva kushindwa kulimudu gari hilo wakati amefika kwenye eneo lenye kona na mteremko mkali," amesema Imori.