CCM yaibuka kidedea Mbarali, Bahati Ndingo atangazwa Mbunge mteule

Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo Mbarali, Missana Kwangura, akikamkabidhi cheti cha ushindi mgombea wa CCM Bahati Ndingo, baada ya kuibuka kidedea katika mchakato huo.
Muktasari:
- Mchakato wa kuhesabu kura za uchaguzi wa Jimbo la Mbarali ulioanza jana bado unaendelea hivi sasa katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali, Missana Kwangura amemtangaza Bahati Ndingo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa mshindi wa katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, ambapo amepata kura 44, 334 dhidi ya mshindani wake wa karibu, Modestus Kilufi wa ACT - Wazalendo, aliyepata kura 10, 014.