Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bunge laahirisha shughuli kujadili wanafunzi kukosa mikopo

Bunge laahirisha shughuli kujadili wanafunzi kukosa mikopo

Muktasari:

  • Bunge limeahirisha shughuli zake kwa muda ili kujadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Biharamulo (CCM) Ezra Chiwelesa ya wanafunzi elimu ya juu waliofaulu vizuri kukosa mkopo.

Dodoma. Bunge limeahirisha shughuli zake kwa muda ili kujadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Biharamulo (CCM), Ezra Chiwelesa ya wanafunzi elimu ya juu waliofaulu vizuri kukosa mkopo.

 Mbunge huyo ametoa hoja hiyo ya dharura baada ya Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kuruhusu ijadiliwa bungeni leo Jumanne Novemba Mosi, 2022.

Chiwelesa amesema juzi walimuona Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akisema kamati aliyoiunda kuchunguza mikopo hiyo imekosa ushirikiano.

“Maana yake Bodi na Serikali haikuwa pamoja ndio maana kamati imekosa ushirikiano, kwa hiyo hilo jambo likanishtua kidogo.

“Mwishoni mwa wiki hii baada ya majina kutoka (waliopata mikopo) nimepata simu nyingi sana wanafunzi wengi wamekosa mikopo na wanakimbilia kwangu,” amesema.

Amesema aliona kuwa kama angerudi kwa Waziri ambaye amemuona katika vyombo vya habari akilalamikia kamati hatajapata ufumbuzi na ndio maana akaona apelike bungeni kama chombo cha wananchi wajadili, hatimaye watoke na maazimio ili waielekeze Serikali nini cha kufanya.

Amesema anamfano wa mtoto wa mkulima aliyesoma shule ya sekondari ya Msalato jijini Dodoma ambaye amepata daraja la kwanza na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya udaktari katika Chuo cha KCMC lakini hajapata mkopo kwa ajili ya kulipia ada.

Amewaomba wabunge kujadili na kuja na ufumbuzi ambao utasaidia kuwakwamua wanafunzi katika jambo hilo na kwamba wako wengine tayari wako vyuoni lakini hawajapata mikopo hiyo.