Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaeleza chanzo vifo vya madereva bodaboda

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Fakharia Shomar Khamis akiuliza swali la nyongeza wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye mkutano wa tisa wa Bunge, jijini Dodoma, Novemba 1, 2022.

Muktasari:

  • Serikali imesema kutovaa kofia ngumu kwa madereva bodaboda ni chanzo kikubwa cha vifo kwa madereva hao kwasababu kichwa kinapogonga barabara ya lami hupasuka ama chombo kingine cha moto.

Dodoma. Serikali imesema kutovaa kofia ngumu kwa madereva bodaboda ni chanzo kikubwa cha vifo kwa madereva hao kwasababu kichwa kinapogonga barabara ya lami hupasuka ama chombo kingine cha moto.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagijini ameyasema leo Novemba Mosi 2022 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Fakharia Shomar Khamis.
Fakharia amehoji Serikali inachukua hatua gani kwa madereva bodaboda ambao hawavai kofia ngumu.
“Kwa hiyo kwa kuepusha haya tunawaelimisha waheshimu sheria, pamoja na kuvaa element (kofia ngumu),”amesema Sajini.
Akiuliza swali la nyongeza Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba alihoji Serikali haioni umuhimu wa kutoa tamko kwa bodaboda wote wanaopita kwenye taa nyekundu, mahali hapana njia na kupakia mishkaki wakamatwe na kuchukua sheria.
Akijibu swali hilo, Sajini amesema trafiki wamekuwa wakichukua hatua kwa makosa hayo lakini mara nyingine kumekuwa na changamoto kwa viongozi wa kisiasa kuwatetea madereva bodaboda.
“Niombe tushirikiane wote, elimu inatolewa, sheria zinachukuliwa lakini tuwe na utashi wa kisiasa wote, madiwani na viongozi wote ili wote tuwe na lugha moja kwa ajili ya usalama wa barabarani, hususani hawa vijana wa bodaboda,”amesema.