Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bundi, ngedere watajwa chanzo treni ya umeme kuchelewa kwa saa mbili

Muktasari:

  • Hitilafu ya umeme kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete ilisababisha treni ya SGR kusimama kwa saa mbili.


Dar es Salaam. Kutokana na hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya SGR iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili njiani huku ngedere, bundi wakitajwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), hitilafu hiyo ilitokea jana Julai 30, 2024.

“Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya WI ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system).

Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) na mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto hiyo na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma ambapo iliwasili mkoani humo saa 7:57 usiku.

Wakati hayo yanajiri kwa upande mwingine, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi safari za treni hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kesho Agosti Mosi.

Awali safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, zilianza Alhamisi Julai 25, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Rais Samia mwishoni mwa mwaka jana, kwamba ifikapo Julai 2024 shirika hilo liwe limeanza safari hizo.

Safari za kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Morogoro zilianza mapema Juni 14, mwaka huu.