Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BoT yaonya wakopaji kwa simu

BoT yaonya wakopaji kwa simu

Muktasari:

  • Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewaonya Watanzania wenye tabia za kuwasajilia laini watu wengine kwa kutumia vitambulisho vyao vya Taifa (Nida) kwamba, watakapotumia laini zao kukopa na kushindwa kulipa watadaiwa wamiliki wa vitambulisho.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewaonya Watanzania wenye tabia za kuwasajilia laini watu wengine kwa kutumia vitambulisho vyao vya Taifa (Nida) kwamba, watakapotumia laini zao kukopa na kushindwa kulipa watadaiwa wamiliki wa vitambulisho.

Hiyo ni kwa sababu watu hao baada ya kusajiliwa laini na kuanza kuzitumia huweza kuzutumia kuchukua mikopo katika mitandao ya simu

Hayo yameelezwa juzi Josephine Temu ambaye ni Mkuu wa kitengo cha uendelezaji biashara kutoka kampuni ya Dun & bradstreet iliyopewa jukumu la ukusanyaji wa taarifa za wakopaji na BoT kutoka benki zote, taasisi za kifedha na kampuni zote zinazotoa mikopo ikiwemo za simu

Akizungumza na Mwananchi juzi katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaaam, alisema kwa sasa usajili wa laini ya simu humtaka mmiliki kuwa na kitambulisho cha Taifa, baadhi ya watu huwasajilia wengine bila kufahamu athari zake.

“Kwa mikopo ya simu unapomsajilia mwenzio namba yake ya simu anaweza kukopa akakimbia ikaja kukupa shida wewe kwa sababu umemsajilia kwa taarifa zako.

“Kampuni itakuripoti wewe kama mkopaji kwa sababu namba yako Nida iliyotumika kusajili ni yako,” alisema Josephine

Hiyo ni kwa wale wenye tabia ya kutumia laini zao kokopa sehemu mbalimbali kwa kutumia simu kama Branch, Timiza, Songesha, Tigo nivushe na huduma nyingine za mikopo zinazotolewa kupitia simu.

Endapo uliyemsajilia atakopa fedha miongoni mwa huduma hizo za kifedha zinazotolewa na kampuni mbalimbali kwa kutumia namba ya simu na akashindwa kulipa basi mmiliki wa kitambulisho ndiyo atakuwa mdaiwa namba moja

Jasiri Kidau ambaye ni mtembeleaji wa maonyesho hayo alishangazwa na taarifa hizo huku akionyesha wasiwasi kuwa huenda anadaiwa.

“Unapomsajilia mtu unakuwa na matumaini atatumia kwa mawasiliano tu sasa inapotokea amekopa na hakulipa deni likawa langu hapo ni pagumu sasa.. kulipa deni ambalo hela yake hukujua ilitumika vipi na huwa inauma sana jambo kama hili,” alisema Kidau.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo imekuwa ikizisaidia benki na taasisi zinazotoa mikopo kupata taarifa za wateja waliopotea na hawajalipa mikopo.