Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biteko ateua wajumbe wapya bodi ya Tanesco

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, Dk Rhimo Nyansaho.

Muktasari:

  • Wajumbe wanane wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wameteuliwa na Dk Biteko ili kuungana na mwenyekiti wao, Dk Nyansaho kuendesha shirika hilo kwa miaka mitatu kuanzia Machi 18, 2024.

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amefanya uteuzi wa wajumbe wanane wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) watakaohudumu kwa miaka mitatu.

Wajumbe hao ni Dk Lucy Mboma, Isaack Chanji, Boma Raballa, Grace Joachim, Profesa Hellen Bandiho, Balozi Zuhura Bundala, Profesa Ninatubu Lema aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ( ERB) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Mwingine ni Idris Kikula, aliyewahi kuwa mwenyekiti Tume ya Madini Tanzania, pia kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Machi 14, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felschesmi Mramba imeeleza hayo huku ikifafanua kuwa uteuzi huo utaanza Jumatatu Machi 18, 2024.

Katika taarifa hiyo, Mramba amesema, Dk Biteko amefikia uamuzi huo baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Dk Rhimo Nyansaho kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco Desemba 19, 2023.

Dk Nyansaho amechukua nafasi ya Meja Jenerali Paul Simuli, aliyetuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.

Dk Nyansaho ni mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa benki ya Azania.

Mramba aliyewahi kuwa bosi wa Tanesco, amesema Dk Biteko amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu namba 19 (1) na (3) cha Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1992.

Bodi iliyopita iliongozwa na mwenyekiti Omary Issa na wajumbe walikuwa Nehemiah Mchechu, Balozi Mwanaid Majaar, Christopher Gachuma, Mhandisi  Cosmas Massawe, Lawrence Mafuru, Zawadi Nanyaro, Abubakar Bakhresa na Abdallah Hashim.