Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benki kuu yaanza kutunza akiba ya dhahabu

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini yanayoendelea mkoani Geita.

Muktasari:

Tanzania imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ipate uhuru baada ya Benki Kuu (BOT) kununua dhahabu na kuihifadhi kwenye mfuko wa kuhifadhi dhamana na hifadhi za nchi wa kimataifa uliopo nchini Uingereza (London)

Geita. Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeandika historia baada ya kuanza kutunza akiba ya nchi kwa dhahabu inayonunuliwa hapa nchini.

Awali benki hiyo ilikuwa ikitunza akiba ya nchi kwa fedha za kigeni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Septemba 23, 2023 katika maonyesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya madini Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba amesema tayari kilo 418 za dhahabu zimenunuliwa tangu benki hiyo ianze kununua madini hayo Septemba 21, mwaka huu.

“Benki kuu tunadhamana ya kusimamia masuala ya ukuaji wa uchumi na uhimilivu wa bei pamoja na mzunguko wa fedha na kwa mara ya kwanza toka nchi ipate Uhuru tulikua tukitunza akiba ya nchi kwa mfumo wa fedha za nje lakini kuanzia juzi tumeingia kwenye historia ya dunia ya kutunza akiba ya nchi kwa dhahabu inayonunuliwa hapa nchini”amesema Tutuba

Amesema dhahabu hiyo inanunuliwa kwa wachimbaji wadogo, wakati, wakubwa na kabla ya kupelekwa kwenye mfuko wa kuhifadhi dhamana husafishwa kwenye viwanda vilivyopo nchini kikiwemo cha GGR kilichopo mjini Geita chenye uwezo wa kusafisha hadi asilimia 99.999 ambayo ni sawa na kutoa dhahabu kwa asilimia 100

Amesema BOT inatumia nafasi kwenye maonyesho hayo kuhamasisha wachimbaji na wafanyabishara wa madini kujua namna watakavyoweza kuuza madini yao kupitia benki kuu.

Tutuba amesema Serikali imefanya maamuzi ya kununua dhahabu ili kuiwezesha nchi kupata fedha za kigeni zitakazowezesha shughuli za kiuchumi lakini pia itakuwa njia mbadala ya kutunza dhamana na akiba ya nchi badala ya kutunza fedha taslimu.

Katika hatua nyingine amewashauri wachimbaji kutumia mifumo ya kielelektoniki kupokea na kutoa fedha badala ya kutembea na fedha taslimu.

“Sisi tunalipa kwa mfumo wa TIPS ambao unarahisisha kwakuwa umeunganisha mabenki yote na miamala ya simu na ndio maana tunawahamasisha watumie mifumo ya kielektroniki kuliko taslimu kwakuwa ni mfumo wa haraka na nafuu utawaepusha na fedha bandia,”amesema

Basil Elias, Mchimbaji mdogo wa dhahabu kutoka Geita amesema uamuzi wa Serikali kununua dhahabu ni fursa pia kwa wachimbaji ambao wataweza kutunza dhahabu zao badala ya kutunza fedha.

“Dhahabu inavyozidi kupanda bei Serikali itapata fedha nyingi kwenye soko la dunia tofauti na kutunza pesa na ni uwekezaji usiotetereka unafaida za haraka ni hifadhi ya uhakika tofauti na dola kuna wakati inashuka thamani “amesema Elias

Akifungua maonesho hayo, Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ameipongeza BOT kwa kuanza kununua zaidi ya kilo 400 zilizosafiswa katika viwanda vya ndani vya kuchenjua dhahabu.

Aidha ameitaka benki hiyo kuwaunga mkono wachimbaji wa madini nchini ili kuleta tija na kuongeza mchango katika Sekta ya Madini.