Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mpenzi wake

Moshi. Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro imemhukumu kunyongwa hadi kufa, Erasto Mollel (32) kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Josephine Mngara (30) kwa kumpiga na jembe kichwani, kisha kuuchoma moto mwili wake kwenye pagale.

Mbali na hukumu hiyo, mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Samweli Mchaki ameachiwa huru na baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha ushiriki wake katika tukio hilo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Machi 10, 2025 na Jaji wa Mahakama hiyo, Adrian Kilimi baada ya kukubaliana na ushahidi dhidi yake uliotolewa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Februari 24, 2025 mbele ya Jaji Kilimi huku upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Kambarage Samson, Frank Ong'eng'a na Grace Kabu.

Erasto Mollel (32) mkazi wa Mtemboni, kata ya Makuyuni, Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro akiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Picha na Omben Daniel

Upande wa utetezi katika kesi hiyo, uliwakilishwa na mawakili Alfredy Sindato Silayo na Lilian Mushi.

Washtakiwa hao kwa pamoja, walikuwa wakishitakiwa kwa kosa la kumuua kwa makusudi, mwanamke huyo kwa kumpiga na jembe huko eneo la Mtemboni, Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Februari 19, mwaka 2023 na kisha kuteketeza mwili wake.

Kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa mashitaka, marehemu alikuwa akiishi na Mollel ambaye alikuwa ni mpenzi wake na aliuawa kikatili usiku wa kuamkia Februari 19, 2023.


Endelea kufuatilia Mwananchi.