Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT- Wazalendo kujaza nafasi za naibu makatibu wakuu

Muktasari:

  • Nafasi za naibu makatibu wakuu wa ACT-Wazalendo (Bara na Zanzibar), huenda zikajazwa siku chache zijazo katika vikao vya juu vya chama hicho vitakavyowateua na kuwathibitisha.

Dar es Salaam. Naibu makatibu wakuu wa chama cha ACT- Wazalendo wa Tanzania Bara na Zanzibar,  huenda wakajulikana ndani ya siku chache zijazo wakati viongozi wakuu wa chama hicho watakapokutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa ACT -Wazalendo wanatarajia kukutana Agosti 23 na 24, 2024 katika kikao cha kamati kuu na kisha halmashauri kuu, katika ofisi za makao makuu ya chama hicho  Magomeni jijini Dar es Salaam.

Taarifa ambazo Mwananchi imezipata kutoka kwa chanzo cha uhakika ndani ya chama hicho, ni kwamba miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa kwenye vikao hivyo ni pamoja na mwenendo wa chama hicho, hali ya siasa, mwenendo wa Serikali ya Umoja ya Kitaifa (SUK) na uteuzi wa naibu makatibu wakuu.

Ikumbukwe kwamba baada ya uchaguzi mkuu wa chama uliofanyika Machi 2024, suala la kuziba nafasi za naibu makatibu wakuu wa Tanzania Bara na Zanzibar liliwekwa kiporo baada ya waliokuwa wakishikilia nafasi hizo, Nassor Ahmed Mazrui (Zanzibar) na Joran Bashange (Bara), kumaliza muda wao.

Hata hivyo, ACT- Wazalendo ilisitisha mchakato wa uteuzi wa nafasi hizo, bila kubainisha sababu za uamuzi huo, badala yake iliwakaimisha watu nafasi hizo hadi sasa.

Wakati uteuzi huo ukisubiriwa kwa hamu, baadhi ya majina ya makada yamekuwa yakitajwa kurithi nafasi hizo.

Miongoni mwa wanaotajwa huenda wakateuliwa na kutihibitishwa na halmashauri kuu ya chama hicho ni pamoja na Mbarala Maharagande, Ester Thomas na  Shaweji Mketo (bara).

Kwa  Zanzibar wanaotajwa ni Salim Bimani anayekaimu kwa sasa unaibu ukatibu mkuu, Mansour Yusuf Himid, Issa Kheri na Mazrui ambaye hata hivyo, aliomba apumzike kutumikia nafasi hiyo.

SUK

Moja ya maazimio yaliyosomwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya ACT-Wazalendo, kilichoketi Machi 2024 ni pamoja na chama hicho, kujitoa katika Serikali hiyo kikidai baadhi ya mambo waliokubaliana hayatekelezwi.

Hata hivyo, kikao hicho kiliagiza uamuzi huo kuwasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Mwananchi lilimtafuta, Naibu Katibu wa Uenezi, Habari na Mawasiliano wa chama hicho,  Shangwe Ayo ambaye alithibitisha uwepo wa vikao hivyo, akisema vitafanyika Agosti 24 na 25 katika ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo katika ofisi za makao makuu ya chama hicho.

“Ni kweli kuna vikao vitakavyojikita katika ajenda za maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji,” amesema Ayo.