Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Wananchi kunyweni kahawa mkuze soko la ndani’

Dar es Salaam. Serikali imewataka wananchi kunywa kahawa Ili kukuza soko la ndani la zao hilo jambo litakalosaidia kuongeza mapato.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa, Primius Kimaryo, alitoa ushauri huo kwenye maadhimisho ya Siku ya Kahawa yanayofanyika kila mwaka nchini.

"Kahawa inayozalishwa nchini inakidhi soko la kimataifa ndomana ndio maana Mwaka huu tumehamasisha wananchi kutumia Kahawa ili kukuza soko la ndani," alisema Kimaryo na kuongeza kuwa Tanzania inazalisha kahawa aina mbili ambazo ni arabika na robusta.

Alisema awali wakulima walikua wanazalisha tani 32,000 kwa mwaka, lakini kutokana na mkakati wa Serikali wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo imesaidia kufikia  tani 82,000 kwa mwaka 2022/2023.

" Serikali ilihamasisha ulimaji wa kahawa kwa kuongeza  uzalishaji wa miche, ili kupata mbegu nyingi ambazo tumesambaza kwa wakulima kwenye mikoa tofauti. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa kuzalisha kutoka tani 32,000 hadi 82,000 kwa msimu wa mwaka 2022/23," alisema.

Alisema wanaendelea kuhamasisha wananchi kuwekeza kwenye vioski vya unywaji wa kahawa kwenye vyuo mbalimbali nchini na migahawa, jambo litakalochangia kuongeza pato la Taifa na kukuza soko la ndani.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye banda hilo walisema ikiwa wananchi wataelimishwa unywaji wa kahawa wanaweza kuongeza pato la Taifa na kukuza soko la ndani.

" Mimi ni mkulima wa Kahawa natoka Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya Serikali kuhamasisha ulimaji wa zao hili limesaidia kuongezeka kwa uzalishaji," amesema Jerome Nkya.

Kwa upande wake, Omary Khamis, mkazi wa Dar es Salaam alisema ikiwa Serikali utatoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utumiaji wa kahawa, soko la ndani litakua.