Waislam kuanza mfungo wa Ramadhani

Muktasari:

  • Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza kesho Alhamisi, Machi 23, 2023 baada ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally kutangaza kuandama kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Dar es Salaam. Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally ametangaza kuanza rasmi kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuanzia kesho, Alhamisi Machi 23, 2023.

"Mwezi umeandama leo Jumatano Machi 23, 2023 na hivyo kuashiria kuwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaanza kesho," amesema Mufti wa Tanzania.

Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar nayo pia imetangaza kuandamwa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Taarifa hiyo imetolewa leo jioni Jumatano, Machi 23, 2023 na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar.

"Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imewataarifu Waislamu wote wa Zanzibar kuwa mwezi umeandama. Hivyo Alhamis Machi 23, 2023 ni sawa na mwezi 1 wa Ramadhan," imesomeka taarifa hiyo ya mwandamo wa mwezi.