Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu gharama kubwa za mbegu nchini zaanikwa

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa mbegu (TOSCI),  Patrick Ngwediagi akizungumza na waandishi wa habari

Muktasari:

  • Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu nchini (TOSCI) imesema gharama kubwa za bei ya mbegu zinatokana na kutokuwepo kwa kifungu cha sheria kinachosimamia bei ya mbegu

Dodoma. Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu nchini (TOSCI) imesema gharama kubwa za bei ya mbegu zinatokana na kutokuwepo kwa kifungu cha sheria kinachosimamia bei ya mbegu japokuwa wanasheria wanaangalia namna ya kukiingiza kifungu hiko.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 15, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Patrick Ngwediagi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa utendaji katika shughuli za taasisi hiyo jijini hapa.

Amesema hakuna chombo chochote kilichopewa mamlaka ya kusimamia suala la mbegu lakini kwa sasa wanasheria wanakuna vichwa kuona namna gani wataliingiza hilo ili kuwasaidia wakulima.

“Serikali inaendelea kutafakari ili waingize vipengele ambavyo vitamfanya mkulima anufaike hususani kwenye bei za mbegu kwani Tanzania inadaiwa kuwa na aina 647 za mbegu,” amesema Ngwediagi.

Akizungumzia ubora wa mbegu amesema wamejitahidi kudhibiti madukani kwenye uingizwaji mbegu bandia licha ya ukweli bado kuna wachache wanaofanya hivyo na siku za hivi karibuni waliwakamata watu watano na kuwapeleka mahakamani ambao TOSCI ilishinda kesi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wakulima wanawake wilaya ya Chamwino, Janeth Nyamayahasi amesema bado kuna kilio kikubwa kuhusu gharama kubwa za kununua mbegu.

 Nyamayahasi ametaja changamoto hizo ni mbegu kupatikana maduka ya mijini pekee ambako wakulima wadogo hawawezi kufika kwa urahisi lakini gharama zake ni kubwa.

“Kingine ni umbali wa kufikiwa, kumbuka mkulima mwenye shamba linalohitaji kilo tatu anaweza kuzifikia mbegu hizo mjini kwa kutumia nauli kubwa wakati wangeweza kuweka mawakala wao hadi vijijini wakatuuzia,” amesema Nyamayahasi.