Russia yasema haijatangaza vifo vya wanajeshi wake

Muktasari:
- Wizara ya Ulinzi nchini Russia leo Jumamosi Februari 26, 2022 imesema haijatangaza vifo vya wanajeshi wake wala majeruhi wanaoshambulia nchini Ukraine
Wizara ya Ulinzi nchini Russia leo Jumamosi Februari 26, 2022 imesema haijatangaza vifo vya wanajeshi wake wala majeruhi wanaoshambulia nchini Ukraine
Jana Serikali ya Ukraine ilitangaza vifo vya wanajeshi wa Russia walioshiriki mashambulizi yanayoendelea hivi sasa nchini humo

Hata hivyo taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa haijatangaza vifo wala majeruhi wa wanajeshi wake bali mashambulizi waliyoyafanya wamepata hasara ya vifaa vya kivita.
Huyu ndiye Rais wa Russia Vladmir Putin
Vita vya Vladmir Putin dhidi ya Ukraine vilianza kiongozi huyo alipokwenda kwenye televisheni ya Taifa na kutangaza “operesheni maalumu ya kijeshi”. Soma zaidi
Putin alitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi wa nchi
Rais wa Russia, Vladimir Putin amelitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi uliopo madarakani wa Rais Volodymyr Zelensky huku akiutuhumu kuwa wa kigaidi na genge la watumiaji wa dawa za kulevya. Soma zaidi