Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Mshahara wa 'housegirl' uwekwe kwenye bahasha’

Muktasari:

  • Waajirii pia wametakiwa kuandika kwa maandishi kila wanapolipa mshahara ili kuweka kumbukumbu hali itakayomwepushia usumbufu pale inapotokea migogoro kati yao.

Dar es Salaam. Imeeelezwa kuwa ni kinyume na sheria kumlipa ujira mfanyakazi bila kuuweka kwenye bahasha.

Sambamba na hilo pia waajiriwa hao wametakiwa kuandika kwa maandishi kila wanapolipwa mshahara ili kuweka kumbukumbu itakayowasaidia  itakapotokea migogoro kati yao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara wa Sheria wa Chama cha Wafanyakazi wa Majumbani Hifadhi, Mahotelini, Huduma za Jamii na Ushauri (Chodawu ), Asteria Gerald alipokuwa akielezea kwa wadau sheria mbalimbali zilizopo katika mkataba wa 189 zinavyohusiana na sheria ya ajira na mahusiano  kazini.

Asteria amesema sheria hiyo imeweka bayana namna mshahara wa mfanyakazi wa ndani unavyopaswa kulipwa ikiwamo kuuweka kwenye bahasha kama unamlipa fedha taslimu.

"Sheria hiyo inasema kama unamlipa fedha taslimu uweke kwenye bahasha na pia umlipe muda wa kazi na mahali pa kazi.

"Hii inafanyika hivyo kwa ajili ya kutengezea mazingira mazuri ya mfanyakazi kupokea mshahara, kwani kuna baadhi ya waajiri wamekuwa wakiwalipa usiku na hivyo kuwaingiza katika vishawishi vingine vya kuwataka kimapenzi," amesema Asteria.

Hata hivyo, mwanasheria huyo amesema katika ulipaji huu wa mishahara ni vema mabosi wakawa wanaweka kumbukumbu ya kimaandishi na kama mfanyakazi hajui kuandika aweke hata dole gumbam, ili uwe ushahidi  ili atakaposema anadai uwe ni uthibitisho.

Kwa upande wao wafanyakazi wa ndani akiwemo Rehema Fadhil, amesema mabosi wengi huwapa fedha taslimu mkononi.

"Tena wakati mwingine bosi unakuta kakuachia mshahara wako juu ya meza ya kulia jikoni au kitandani kwako, hivyo wanachosema Chodawu ni kweli kabisa ifike mahali tuheshimiwe kama wafanyakazi wengine," amesema Rehema. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Majumbani, Zanini Othuman amesema suala la mikataba kwa wafanyakazi limekuwa pasua kichwa kwani hata katika baadhi ya mikoa ambayo wamefanya mafunzo, wamekuta wafanyakazi wasiozidi 10 ndio wenye mikataba.

"Katika kuhamasisha uwepo wa mikataba  tumejipanga walau hadi kufika 2024 kuwepo na mikataba mipya 2,000 itakayosainiwa kati ya waajiri na wafanyakazi wao," amesema Zanini. Naye Ofisa Ustawi Jiji la Dar es Salaam, Joyce Maketa, amesema wamekuwa wakipokea malalamiko ya aina hiyo na inaposhindikana kuyasuluhisha huyapeleka Tume ya Usuluhishi ya Kazi.