Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matano ya kuangalia uchaguzi wa Russia leo

Muktasari:

Wananchi wa Russia leo wanapiga kura za kuchagua viongozi wa mikoa na manispaa ikiwa ni wiki kadhaa baada ya polisi kupambana na wanasiasa ambao walionekana wangegombea kama wagombea binafsi.

Moscow, Russia. Wananchi wa Russia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa mitaa na mikoa. Uchaguzi katika manispaa na mikoa umefanyika leo, lakini macho yameelekezwa katika bunge la Moscow kutokana na kukamatwa kwa wagombea ambao wangesimama bila ya vyama. Haya ni mambo matano ya kuangalia katika uchaguzi huo utakaofanyika katika mikoa 85

 Jinsi serikali inavyokubalika 
Uchaguzi wa Gubernatorial au wa magavana utafanyika katika mikoa 16. Uchaguzi kwa ajili kwa ajili ya kupata wabunge utafanyika katika maeneo 13, ikiwemo Crimea ambayo Russia ililichukua kutoka Ukraine mwaka 2014.
Wapigakura wa Russia, wakipambana na umaskini unaongezeka kutokana na vikwazo ambayo nchi yaoe imewekewa na mataifa ya Magharibi pamoja na mageuzi tata ya mfumo wa pensheni, wanazidi kuwa na nia ya kuwaadhibu wawakilishi wa chama tawala cha United Russia.
Wagombea wengi ambao wanaiunga mkono serikali wanajifanya ni wagombea huru katika jitihada za kujitofautisha na chama, ambacho sasa kinaonekana kuwa mzigo.
wagombea sita kati ya 16 wanaowania kurejea katika nafasi zao au kuingia madarakani wamepiga kampeni wakijitambulisha kama wagombea huru.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema uchaguzi utakuwa mtihani muhimu dhidi ya uwezo wa mamlaka kuendesha uchaguzi baada ya Rais Vladmir Puting kupoteza idadi kubw aya watu wanaomuunga mkono.

Hatari ya kwenda raundi ya pili
Wafuatiliaji wa uchaguzi wanaona kuna uwezekano kuwa wanachama wa chama tawala wanaweza wasipate ushindi wa moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa magavana katika baadhi ya maeneo.
Mwaka jana, serikali ilipata pigo kubwa katika maeneo manne ambako wagombea wa chama tawala walishindwa kupata ushindi wa moja kwa moja katika raundi ya kwanza.
Katika eneo la mashariki la Primorsky Krai, madai ya ukiukwaji wa taratibu kwa lengo la kusaidia wagombea wa chama tawala, yalilazimisha wasimamizi warudie upigaji kura, jambo ambalo ni nadra sana, mwaka 2018. Hata hivyo, mgombea wa chama tawala alishinda.

'Upigaji kura makini'
Uchaguzi wa wabunge utakuwa mtihani dhidi ya uwezo wa mkosoaji mkubwa wa serikali, Alexei Navalny wa kushawishi wapinzani kabla ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2021 baada ya polisi kuwashughulikia katikati ya mwaka.
Wagombea maarufu wa upinzani wamezuiwa kugombea Moscow na Navalny amewashauri wakazi wa Moscow kuunga mkono wale walio na nafasi kubwa ya kuwaangusha wagombea wanaoiunga mkono serikali -- wengi wao wakomunisti.
Navalny pia ameshauri wakazi wa miji mingine kupiga kura kimkakati.
Kuwafanya wafuate mwongozo wake, timu ya Navalny katika siku za karibuni imekuwa ikifanya uchunguzi kila siku, ikituhumu viongozi maarufu kwa kujihusisha na rushwa.

Kura za Saint Petersburg
Gavana ambaye hapendwi, Alexander Beglov, rafiki wa muda mrefu wa Putin, anategemewa kupata ushindi bila vikwazo kutokana na kukosa ushindani wa maana.
Lakini ukubwa wa ushindi wake bado haujulikani na wapinzani wamedai kuwa mamlaka zinajiandaa kupika matokeo ya uchaguzi wa mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Russia.
Gazeti la upinzani la Novaya Gazeta liliripoti wiki hii kwamba baadhi ya maofisa wa uchaguzi kutoka mji huo wa nyumbani kwa Putin wamepewa mafunzo ya ya kuingiza kura feki "katika dakika za mwisho".
"Kila kura nyingine ya A iende kwa B," liliripoti gazeti la Novaya Gazeta likimkariri mkufunzi.
Mpinzani mkubwa wa Beglov ambaye ni dikteta na mbunge wa enzi za Urusi na Mkomunisti, Vladimir Bortko, alijiondoa bila ya kutarajiwa kabla ya upigaji kura.

 Mkoa wa Khabarovsk
Mkoa ulio mashariki ya mbali wa Khabarovsk ni sehemu ambayo chama cha United Russia kimepigana moja ya vita zake ngumu mwaka huu.
Mkoa huo ulioko mpakani na China utakuwa na uchaguzi wa kumpata mbunge, madiwani wa jiji na meya.
Gavana wa Khabarovsk, Sergei Furgal wa chama cha LDPR aliingia madarakani kwa ushindi mkubwa mwaka jana, akipata asilimia 70 ya kura dhidi ya Vyacheslav Shport, aliyekuwa akitetea nafasi.
Furgal, 49, ameondokea kuwa kiongozi maarufu wa mkoa, akipambana na urasimu na amekusanya wafuasi 161,000 katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram.
Wakazi wengi wanajiandaa kuiunga mkono LDPR ambayo sasa wanaihusisha zaidi na Furgal kuliko kiongozi mtata wa zamani, Vladimir Zhirinovsky.
Kutokana na ushindi wa Furgal mwaka jana, chama tawala cha United Russia sasa kimekuwa cha upinzani katika mkoa huo.