Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinondoni yajipanga mikopo ya asilimia 10

Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi benki ya DCB, Emmanuel Barenga (kulia) akimkabidhi viti, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (wapili kushoto) kwa ajili ya wajasiriamali wadogo waliopo katika viwanda vidogo vidogo vya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk Peter Nsanya. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Benki ya Biashara ya DCB imetoa msaada wa viti na meza kwa Halmashauri ya Kinondoni ili kuwezesha utekezaji wa majukumu yake hususan utoaji wa mikopo ya asilimia 10.

Dar es Salaam. Ikiwa ni njia moja wapo ya kuchochea huduma bora kwa wananchi, idara ya maendeleo ya jamii kitengo cha mikopo ya asilimia 10 wa manispaa ya Kinondoni wamepokea misaada ya viti 60 na meza moja ili kuiwezesha idara hiyo kuwa na mazingira rafiki wakati wa utendaji wao wa kazi.

Akipokea misaada hiyo leo Alhamisi, Januari 16, 2025 kutoka Benki ya Biashara ya DCB, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amesema moja ya majukumu ya idara hiyo ni kuchakata mikopo.

“Dhima ya idara hii ni kuchakata mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wajasiriamali ambapo vijana wanapata asilimia 4, kinamama asilimia 4 na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu, na kuwa uchakataji wa mikopo hiyo unahitaji mahali tulivu na mazingira rafiki kwa utendaji bora wa kazi,” alisema.

Mnyonge alisema Manispaa ya Kinondoni imeteua ukumbi wa eneo la viwanda vidogo vya Mwananyamala kuwa makutano ya maofisa ustawi wa jamii ili kufanya kazi zao za kutoa mikopo hiyo.

“Tulikuwa na upungufu wa viti, uongozi wa manispaa ukawabipu benki hii na benki  ikatupigia kwa kutusaidia msaada huu wa viti,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa benki hiyo, Emmanuel Barenge amesema mpaka hivi, mbali na misaada mbalimbali wanayotoa, wameweza kutoa mikopo ya Sh bilioni 5 kwa kina mama na vijana.

“Mpaka sasa tumetoa Sh5 bilioni kwa kina mama na tumelenga kufikia kiasi cha zaidi ya bilioni 15 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2025, huku lengo, likiwa ni kuwainua vijana na kinamama kiuchumi,” alisema.

Burenge alisema, moja ya mikakati ya benki hiyo tangu kuanzishwa kwake ni kutoa gawio kwa manispaa za jiji la Dar es Saalam ambao ni wamiliki wa benki hiyo kwa asilimia 45.

“Kwa mwaka jana, tumetoa gawio la zaidi ya Sh4.2 bilioni kwa manispaa za Jiji la Dar es Salaam,” alisema.

Kadhalika mwenyekiti wa umoja wa vikundi vyote vinavyosaidiwa ndani ya manispaa ya kinondoni, Seif Jumanne amesema moja ya changamoto waliyokabiliana nayo ni pamoja na ukosefu wa eneo la kufanyia shughuli zao na viti.


“Kabla ya kupokea msaada huu tulikua na changamoto ya ukosefu wa sehemu ya kufanyia mikutano na uchambuaji wa katiba,”anaeleza

Jumanne alisema tatizo hilo walilifikisha kwa halmashauri na sasa wamepata msaada.

“Halmashauri hii inajua namna ilivyohangaika mpaka kupata msaada huu ambapo kwa namna moja au nyingine itaongeza utendaji kazi,” alieleza.

Sambamba na hilo, mwenyekiti huyo aliiishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kutatua changamoto ya viti, na kusisitiza wadau wengine kuiga mfano huo ili kupata maendeleo na kuongeza utendaji kazi.