Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

24 wapoteza maisha katika ajali ya gari Kenya

Muktasari:

  • Ajali hiyo iliyohusisha basi la kubeba abiria na lori la kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kiambu, karibu na Mtito Andei.
  • Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard Kimaiyo ameambia BBC kuwa watu 23 walifariki papo hapo na mwingine mmoja alifariki alipokuwa akipata matibabu.

Nairobi. Watu 24 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa manane katika barabara kuu ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Ajali hiyo iliyohusisha basi la kubeba abiria na lori la kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kiambu, karibu na Mtito Andei.

Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard Kimaiyo ameambia BBC kuwa watu 23 walifariki papo hapo na mwingine mmoja alifariki alipokuwa akipata matibabu.

Watu 20 walipata majeraha na kupelekwa katika hospitali za miji ya Kibwezi na Makindu.

 Kimaiyo amesema walionusurika waliwaambia maofisa wa polisi kuwa dereva wa basi alikuwa akijaribu kupita gari jingine na kusababisha basi hilo kugongana na lori hilo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi Kenya, watu 3,000 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.